` MHANDISI JAMES JUMBE AREJESHA FOMU YA UBUNGE JIMBO LA SHINYANGA MJINI

MHANDISI JAMES JUMBE AREJESHA FOMU YA UBUNGE JIMBO LA SHINYANGA MJINI

MHANDISI JAMES JUMBE AREJESHA FOMU YA UBUNGE JIMBO LA SHINYANGA MJINI

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MHANDISI James Jumbe Wiswa, amerejesha Fomu ya kuomba Ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)kumteuwa kugombea Ubunge katika Jimbo la Shinyanga Mjini.

Amerejesha Fomu hiyo leo Julai 2,2025 katika Ofisi za Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini.

Akizungumza mara baada ya kurejesha Fomu hiyo,amesema zoezi limekwenda vizuri,huku akieleza kufurahishwa na mazingira Rafiki ya Wagombea namna ya kuchukua Fomu na kurudisha.

"Napongeza Ofisi za Chama, wameweka mazingira Rafiki ya Wagombea kuchuka Fomu na zoezi limekwenda vizuri na sasa tunasubili taratibu zingine za kichama,"amesema Mhandisi Jumbe.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464