` SAKALA AJITOSA UDIWANI KATA YA MJINI

SAKALA AJITOSA UDIWANI KATA YA MJINI


Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini Abdulaziz Said Sakala,amechukua Fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa na Chama chake cha CCM kupeperusha bendera kugombea Udiwani katika Kata ya Mjini Manispaa ya Shinyanga uchaguzi Mkuu 2025.

Amechukua Fomu hiyo leo Juni 30,2025 kwenye Ofisi za CCM Kata ya Mjini na kukabidhiwa na Katibu wa CCM Kata hiyo Rashid Abdalla.

Akizungumza mara baada ya kuchukua Fomu hiyo, amesema yeye kama kijana ameamua kutumia haki yake ya Kikatiba kuchukua Fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea nafasi hiyo ya Udiwani.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini Abdulaziz Said Sakala (kulia)akikabidhiwa Fomu ya kugombea Udiwani Kata ya Mjini na Katibu wa CCM Kata hiyo Rashidi Abdalla.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464