MISA-TANZANIA YAKUTANA NA MKURUGENZI MKAZI WA UNESCO MICHEL TOTO WAJADILI MASUALA MBALIMBALI YA TASNIA YA HABARI
Na Marco Maduhu,ARUSHA
BAADHI ya Wanachama wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA TAN) Tawi la Tanzania, wamekutana na Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO Nchini Tanzania Michel Toto, katika hafla ya kuadhimisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani.
Mwenyekiti wa Misa-Tanzania Edwin Soko (kushoto)akiwa na Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO Nchini Tanzania Michel Toto.
Mkutano huo ulifanyika kwa lengo la kuendeleza majadiliano kuhusu hali ya uhuru wa vyombo vya habari nchini Tanzania na kuimarisha ushirikiano kati ya wadau wa habari na mashirika ya kimataifa kama UNESCO.
Katika majadiliano yao, wamegusia changamoto zinazoikumba sekta ya habari, ikiwemo mazingira ya kazi kwa wanahabari, pia umuhimu wa kuwalinda wanahabari na kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa uhuru na usalama.
Aidha, wametafakari pia fursa zilizopo kwa maendeleo ya tasnia ya habari kupitia matumizi ya teknolojia ya kisasa, mafunzo endelevu kwa wanahabari, pamoja na uimarishaji wa misingi ya maadili ya taaluma ya uandishi wa habari.
Ushirikiano na mashirika kama UNESCO umetajwa kuwa nguzo muhimu katika kufanikisha malengo hayo ya Tasnia ya Habari.
Baadhi ya wanachama wa Misa-Tanzania wakipiga picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkazi ya UNESCO Michel Toto.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464