Header Ads Widget

WADAU WATAKA STADI ZA MALEZI NA MAKUZI YA WATOTO KUPEWA KIPAUMBELE


Washiriki wa kikao wakiwa katika kikao cha uwasilishaji taarifa ya utafiti wa tathimini ya stadi za maisha na maadili kwa vijana (13-17) wilayani Kahama

Meneja wa shirika lisilo la kiserkali la TADEPA Penina Petro(aliyesimama) akiwasilisha taarifa ya utafiti wa tathimini ya stadi za maisha na maadili kwa vijana (13-17) wilayani Kahama.

Na Elizabeth Charles

WADAU wilayani Kahama mkoani hapa wameshauri jamii,viongozi wa dini pamoja na serikali  kuandaa mikakati ya pamoja katika malezi na makuzi ya watoto lengo ikiwa ni kusaidia kukuza viwango vya stadi za maisha  na maadili.

Hayo yamebainishwa jana tarehe 25/05/2023  katika uzinduzi wa taarifa ya mradi wa ALIVE wenye lengo kupima uwezo wa stadi za maisha kwa vijana wenye umri kati ya miaka 13-17 wilayani Kahama yanayotekelezwa na shirika lisilo la kiserkali la Milele Zanzibar Foundation kushirikiana na shirika la TADEPA Kahama.

Akizungumza katika hafla hiyo meneja wa shirika lisilo la kiserikali la TADEPA Penina Petro amesema utafiti umeonesha kuwa watoto wengi bado hawajitambui hali ambayo inawasababisha kushindwa kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.

“Kuna uhitaji mkubwa wa wazazi kuwekeza kwenye malezi na makuzi ya watoto wao lakini pia walimu kule shuleni waendelee kuwafundisha na kuwaelekeza mambo mazuri  pia jamii inawajibu wa kushirirkiana na wazazi kulea kwasababu watoto kwa sehemu kubwa wanashinda na  katika michezo mbalimbali” amesema Penina.

Kwa upande wake Mwezeshaji katika mradi wa upimaji wa stadi za maisha(ALIVE)Husna Kingu amesema vijana wengi hawana mahiri za stadi za maisha na maadili  ambazo ni kujitambua,kutatua matatizo,ushirikiano na maadili ya heshima hivyo kama jamii inatakiwa kuinuka kusaidia watoto.

Afisa maendeleo ya jamii manispaa ya Kahama Robert Kwela amesema watashirikiana na maafisa elimu msingi waende wakaangalie tatizo liko wapi kwenye ufundishaji.

“Tutaelekezana mpaka na wenzetu kwenye idara ya maendeleo ya jamii na wao washuke kwenye ngazi ya kaya   wakusanye taarifa  nafikiri tutajua wapi kuna tatizo”alisema kwela.

Mwakilishi wa katibu tawala wilaya ya Kahama Vicent Ndesekio amewataka viongozi kuanzia ngazi ya kata na serikali za mitaa kuandaa utaratibu wa kuzungumza na wazazi na walezi kuhamashisha malezi bora katika familia.

Aidha miongoni mwa mambo yaliyobainishwa kupitia taarifa ya utafiti wa Mashirika hayo  ni pamoja na asilimia 68 ya vijana  kati ya umri wa miaka 13-17 wilayani Kahama hawana umahiri wa kusoma na stadi za maisha.

Mwezeshaji katika mradi wa upimaji wa stadi za maisha(ALIVE)Husna Kingu akichangia mada katika mkutano wa uwasilishaji taarifa ya utafiti wa stadi za maisha na maadili kwa vijana (13-17 )wilayani Kahama



Afisa maendeleo ya jamii manispaa ya Kahama Robert Kwela akizungumza katika kikao cha uwasilishaji wa taarifa ya utafiti wa tathimini ya stadi za maisha na maadili kwa vijana (13-17 ) wilayani Kahama

Mwakilishi wa katibu tawala wilaya ya Kahama Vicent Ndesekio akizungumza katika kikao cha uwasilishaji taarifa ya utafiti wa tathimini ya stadi za maisha na maadili kwa vijana (13-17) wilayani Kahama

Washiriki wa kikao wakifuatilia uwasilishaji taarifa ya utafiti wa tathimini ya stadi za maisha na maadili kwa vijana (13-17) wilayani Kahama

Washiriki wa kikao wakifuatilia uwasilishaji taarifa ya utafiti wa tathimini ya stadi za maisha na maadili kwa vijana (13-17) wilayani Kahama






Post a Comment

0 Comments