Header Ads Widget

POLISI SHINYANGA YAKAMATA MADEREVA 932 KWA UKIUKWAJI SHERIA ZA USALAMA BARABARANI.

 POLISI SHINYANGA YAKAMATA MADEREVA 932 KWA UKIUKWAJI SHERIA ZA USALAMA BARABARANI.


Kamanda wa jeshi la polisi mkoani hapa  ACP Janeth S. Magomi

Na Mwandishi wetu.

JESHI la  polisi mkoani Shinyanga limewakamata madereva 932  kwa   madai ya makosa ya uvunjifu wa sheria za usalama barabarani katika kipindi cha mwezi mmoja  kupitia oparesheni ya kukamata maderava wanaokiuka sheria za usalama barabarani.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani hapa  ACP Janeth S. Magomi,ameleza hayo  leo mei 25,2023 katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.

Kamanda Magomi amesema katika  opareshi hiyo  wamehakikisha  kuthibiti matukio hatarishi yanayosababisha ajali za mara kwa mara na kufanikiwa kukamata Magari  944 yaliyokiuka sheria za usalama barabarani hasa makosa ya mwendokasi.

“Madereva 11 wa kampuni mbalimbali za mabasi ya kubeba abiria wamefikishwa mahakamani kwa mwendokasi kati ya 90kph na 99kph na maderva 932 walikamatwa kwa kutumia speed radar na VTS wakiwa kwenye mwendokasi kati ya 80kph na 89kph na kuandikiwa faini.”amesema  Magomi.

Jeshi la polisi  pia  limekamata gari mbili aina ya Toyota Hiace yenye  namba za usajili  T202BTW na T358DKM kwa kosa la kughushi nyaraka  za serikali kitendo ambacho ki kinyume na sheria.

Kamanda  Magomi amesema  wamefanikiwa kukamata mirungi bando 24, bangi  kete 206, viti  vya plastiki  vinne ,vigae box 8,betri za mnara ya simu02,pikipiki 05,mahine za kurandia mbao mbili,redio tatu na ng’ombe 13,TV-nane,baiskeli mbili ,vifaa vya kupigia ramli,mbao nane,pampu ya maji moja ,mabati 19,vipande vya chuma saba  na msumeno mmoja .

Aidha,Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limetoa wito wa wananchi kufuata sheria za nchi na kutojihusisha na vitendo vya uhalifu.

Jeshi limewataka madereva kutii na kuheshimu alama,michoro na sheria za barabarani wakati wote na halitosita kumchukulia mtu au kikundi cha watu hatua kali za kisheria kwa yeyote atakae jihusisha na vitendo vya uhalifu”Anasema magomi.


Post a Comment

0 Comments