Header Ads Widget

MADIWANI WAOMBA WAKULIMA KUSOGEZEWA MBOLEA KARIBU NA MAENEO YAO


Mkurugenzi wa halmashauri ya Ushetu Linno Mwageni akiwa na makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo kwenye kikao cha kawaida cha baraza la amdiwani  wakisikiliza hoja.

Na  Kareny  Masasy,Ushetu

BAADHI ya madiwani   wa halmashauri ya Ushetu  wilayani Kahama mkoani Shinyanga  wameomba  wakulima kusogezewa  mbolea  ya ruzuku  karibu  na maeneo yao  ili kuepuka gharama kubwa ya kusafiri kufuata mboleo  hiyo kwa mawakala.

Wakiongea kwenye kikao cha kawaida cha  baraza la madiwani hapo jana  diwani viti maalum Felister  Kabasa na diwani wa kata ya Mapamba Yohana  Emanuel walitoa  hoja hiyo.

 “Mbolea ya ruzuku imekuja  lakini  wakulima wanapata changamoto ya kuifuata  wanaiomba serikali kuliangalia hilo  limeanza kuwakatisha tamaa wakulima”amesema  diwani Kabasa.

Makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo  Doa Limbu amesema changamoto ya  umbali kufuata mbolea za ruzuku na ucheleweshaji wa mbegu za pamba ufanyiwe kazi  kwani kilimo ni sasa na izingatiwe idadi.

Ofisa kilimo wa halmashauri  hiyo Deus Kakulima amesema wameongea na mawakala wanaotoa mbolea hiyo nakukubaliana  kusogea karibu kuwe na vituo sita.

 Madiwani hao   wamelalamikia  pia  kushindwa kufanyika shughuli za maendeleo katika robo mbili za mwaka kutokana na mfumo  wa kuhamisha fedha kushindwa  kufunguka.

 Diwani kutoka kata ya Kisuke  Joseph Bundala na diwani kutoka kata kinamapuka Samweli Sharifu walitoa  hoja hiyo  katika kikao Cha baraza la madiwani.

Makamu mwenyekiti wa halmashauri  hiyo Doa Limbu amesema wamekuwa wakihitaji maendeleo  lakini suala la mfumo  limeonekana kukwamisha na liko nje ya uwezo wa halmashauri.

Mwekahazina  wa halmashauri hiyo Prosper Mlacha amesema   hakuna mfumo wa halmashauri ya Ushetu bali mfumo  huo unatumika kwa nchi nzima na unasimamiwa na Tawala za mikoa na serikali za mitaa (Tamisemi) na umekuwa ukileta changamoto .

Madiwani  wa halmashauri ya Ushetu wakiwa kwenye kikao cha baraza  la  madiwani 

Mkurugenzi wa halmashauri  ya Ushetu Linno Mwageni akijibu hoja kwenye kikao cha baraza la  madiwani.

Post a Comment

0 Comments