Header Ads Widget

MAKADA WA CHADEMA WALIOHUKUMIWA KWA WIZI NA UBAKAJI WAACHIWA HURU


 Na Mwandishi Wetu, SHINYANGA

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga imewachiwa huru makada wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambao walihukumiwa kifugo cha maisha Jela kwa makosa ya wizi, unyang'anyi wa kutumia silaha na ubakaji.

Makada hao ni Katala Kikaja na Ng'hulima Lilanga


Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga Athuman Matuma ametoa uamuzi Jana
  baada ya kuridhika na hoja za warufani kuwa ushahidi uliowatia hatiani Aprili 12, mwaka huu, ulikuwa dhaifu, unaotia mashaka na usiokubalika mbele ya sheria.

Wana Chadema walitiwa hatiani kwa makosa mawili ya wizi, ubakaji, kuharibu mali na unyang’anyi wa kutumia silaha baada ya kukamatwa wakiwa kituo cha kupigia kura Kata ya Dutwa Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu walikokuwa mawakala wa wagombea wa chama hicho katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, 2020. 
 
Mbali na wizi wa Sh300, 000, Makada hao pia ileelezwa kuwa walimbaka msadizi wa kituo cha kupigia kura ambaye jina lake lilihifadhiwa.

Post a Comment

0 Comments