Header Ads Widget

MBUNGE KISHAPU AWATAKA WANANCHI WALIO ATHIRIKA NA MAJITOPE YA MGODI WA MWADUI WILLIAMSON KUWA WATULIVU KUSUBILI STAHIKI ZAO



Mbunge wa jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akizungumza na wananchi


Suzy Luhende, Shinyanga Blog


Kishapu. Mbunge wa Kishapu Boniphace Butondo amewataka wananchi walioathirika na maji tope kuendelea kuwa na utulivu, na imani kwamba mgodi wa almasi wa Williamson Diamond Ltd (WDL) utaendelea kuwahudumia huduma zote zinazotakiwa za kibinadamu, na kuhakikisha unawalipa haki zao zote zinazotakiwa baada ya taratibu kukamilika.


Hayo ameyasema leo wakati alipokuwa ameenda kwa ajili ya kuwajulia hali na kuona maendeleo yao, ambapo amewataka waendelee kuwa na utulivu ili waweze kupatiwa sitahiki zao zote wanazotakiwa kupewa, ila waendelee kuhudumiwa vizuri na kujali afya zao.


Butondo amesema serikali inawajali wananchi wake hivyo itahakikisha inasimamia kikamilifu ili waweze kupata sitahiki zao na watajengewa nyumba za kuishi, ambazo zitakuwa bora na salama, na nyumba hizo zitajengwa kulingana na familia zilivyo.


"Licha ya kujengewa nyumba pia mtalipwa sitahiki zenu zote na sasa mgodi unaendelea kufanya taratibu za kutafuta nyumba za kupangisha zinazozunguka mgodi huu kwa wale watakaotaka kwenda kuishi huko mtahudumiwa kama kawaida huku taratibu za ujenzi zikiendelea na kutafutiwa eneo kwa ajili ya kulima kwa sababu maeneo yenu mliyokuwa mnalima yamevamiwa na tope ambalo mpaka sasa hivi bado bichi,"amesema Butondo.


"Nilipokuja awamu ya kwanza niliwaahidi kuwa nitakuja tena kuwaona mnaendeleaje ndiyo maana nimekuja, nilisisitiza mpatiwe huduma nzuri na salama, ninaamini mnatendewa haki na mnapata chakula vizuri na sisi ndio tunataka mpate chakula kizuri ili muendelee kupata amani kama watu wengine,"amesema Butondo.


Mbunge huyo pia aliushukuru uongozi wa mgodi huo kwa kuendelea kuwahudumia wananchi hao na kuwapeleka shule na kuwarudisha wanafunzi walioathirika na majitope, hivyo amewataka waendelee kuwahudumia na kuwapeleka shule, ikiwa ni pamoja na kuwanunulia sare za shule na viatu ili wajisikie vizuri.


"Serikali ipo pamoja na ninyi inawapa pole sana,kwa kupatwa na ajali hii, sio kwamba mnapenda kukaa hapa ni kwa sababu ya shida tu, hapa mnakaa kama vile mpo kifungoni hamfurahi sana ,hivyo tunaomba taratibu hizi zifanyike kwa haraka ili muende kwenye nyumba zenu ambazo zitajengwa na kukamilika ndani ya miezi minne ama mitano, maisha ya hapa si sawa na yale mliyokuwa mnaishi awali,"ameongeza.


Afisa mahusiano wa mgodi huo Benard Mihayo amesema wananchi hao wametoka katika kijiji cha Kabondo kata ya Mwadui Lohumbo baada ya kupatwa na janga la ajali ya majitope wapo watu 131 na kaya 32 hivyo wanawahudumia chakula sehemu ya kulala wanafunzi 36 wanawapa chakula cha kwenda nacho shule wanawapeleka shuleni na kuwa


"Hakuna atakayedhulumiwa chochote kwani kutakuwa na timu ya kijiji na ya serikali ili kuhakikisha mwananchi anachokiongea ni sahihi, tathimini ndio itatuongoza ili kuhakikikisha mwananchi anapata sitahiki zake hivyo nawaomba muendelee na uvumilivu, sisi tutahakikisha mnapata huduma zote mnazositahili, na kwa sasa hatuendelei na uzalishaji mpaka pale serikali itakapomaliza uchunguzi wake ndipo utaanza uzalishaji, amesema Mihayo.


Kwa upande wake meneja wa mgodi huo Ayoub Mwenda alisema sualala la kwamba watalipwa lini wawaachie watu wa tathimini ili kuhakikisha kila mtu analipwa anachostahili,na eneo hilo wanaloishi kwa sasa wataliboresha, na kwa yule anayependa kwenda kule watahakikisha wana mhudumia kama wanavyomhudumia kwa sasa, kwa sababu ni wajibu wao.


"Tutaongea na viongozi wa kijiji wa wilaya ili mpate maeneo ya karibu mnayoyazoea na kuhakikisha watoto wanaenda shule,tunatakiwa tupate idadi ya watu wote, hii ni ajali ambayo hakuna aliyekusudia mpaka sasa hivi hakuna anayejua kuwa chanzo ni nini, hivyo uchunguzi unaendelea ili kujua chanzo ni nini tuwe na uvumilivu tupo pamoja nanyi bega kwa bega,"amesema Mwenda.


Baadhi ya wananchi wamesema changamoto zao, Robart Gibe amesema kuna baadhi ya watu walisema kuwa wasijengewe nyumba wapewe fedha zao na wengine wajengewe, aliomba hoja hiyo iingizwe kwenye mazungumzo ili kila mtu atoe maamuzi ama ajengewe ama alipwe fedha.


Hata hivyo waathirika hao wa majitope bado wapo mgodini wanaendelea kuhudumiwa,na pia wanaendelea vizuri, wale watoto waliokuwa wamelazwa hospitali wameshapona wapo hapo mgonidi, na maisha yao kwa sasa wanategemea kuhudumiwa kwa kila kitu wanachohitaji, wengine waliopoteza mawasiliano zimenunuliwa simu mbili kwa ajili ya mawasiliano moja kwa wanawake na moja kwa wanaume.


Tunamshukuru Mungu kwa kweli tunaendelea vizuri hakuna aliyepata madhara kuhusiana na maji haya, mifugo nayo haijaathirika, labda kuna baadhi ya kuku zilipotea na maji na baadhi ya mbuzi ambazo idadi yake haijajulikana ila wamesema tutaorodhesha vyote vilivyopotea tutalipwa amesema Gibe mmoja wa waathirika hao.


Mbunge huyo pia aliambatana na viongozi mbalimbali wakiwemo viongozi wa chama cha mapinduzi CCM, ambao ni mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM wilaya Shija Ntelezu, Edward Ngelela mwenyekiti wa Shinyanga na katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga.


Mbunge wa jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akizungumza na wananchi walioathirika na majitope


Katibu wa chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga ambaye aliambatana na mbunge kwa ajili ya kuwajulia hali

Mbunge wa jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akizungumza na wananchi


Meneja wa mgodi wa Mwadui Williamson Diamond Ayoub Mwenda akitoa ufafanuzi wa malipo ya wananchi walioathrika na maji tope kwa mbunge





Mbunge wa jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akitafakari jambo








Meneja wa mgodi wa Mwadui Williamson Diamond Ayoub Mwenda katikati ni Mbunge wa jimbo la Kishapu Boniphace Butondo na kushoto ni meneja uhusiano wa mgodi huo Benard Mihayo
Mbunge wa jimbo la Kishapu akizungumza na wafanyakazi wa mgodi huo katika eneo lililoathirika na majitope ambako tayari wanaendelea kutengenezea maji hayo ili yasiendelee kutiririka










Wananchi walioathirika na majitope wakiwa kwenye picha ya pamoja katika makazi yao wanayoishi mgodini hapo baada ya mazungumzo


Wananchi wakimsikiliza Mbunge wa jimbo la Kishapu Boniphace Butondo

Mmoja wa waathirika akiuliza jambo

Mmoja wa wananchi akichangia jambo baada ya mbunge kuzungumza na kuwatia moyo kuwa serikali ipo pamoja nao

Mmoja wa wananchi akiulizia kama watalipwa sitahiki zao baada ya hapo

Post a Comment

0 Comments