Header Ads Widget

WATUMISHI 1,477 WASIMAMISHWA KAZI

WATUMISHI 1,477 WASIMAMISHWA KAZI
Naibu Waziri katika Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Deogratius Ndejembi amesema watumishi wa umma 1,477 wamesimamishwa kazi kwa kukiuka sheria, kanuni, taratibu na miongozo inayosimamia nidhamu katika utumishi wa umma
 
Ndejembi ameyasema hayo leo Jumatatu Aprili 11, 2022 wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mlimba (CCM), Godwin Kunambi.

Kunambi ameuliza namna mashauri yanayoendelea kusikilizwa na Tume ya Utumishi wa Umma yanachukua muda mrefu sana.

“Nini mkakati wa Serikali kuhakikisha kuwa mashauri haya yanakamilika kwa wakati?,”amehoji Kunambi.
 
SOMA HAPA ZAIDI CHANZO MWANANCHI.

Post a Comment

0 Comments