Header Ads Widget

WAKULIMA WA TUMBAKU KAHAMA WALALAMIKIA BEI NDOGO YA UNUNUZI WA ZAO HILO IKILINGANISHWA NA GHARAMA ZA KILIMO

Mwenyekiti wa Chama kikuu cha Ushirika cha Wilaya ya Kahama (KACU ) Hamis Majogoro akiongea katika mkutano maalumu wa viongozi wa vyama vya msingi (AMCOS) vya tumbaku vya ushirika huo juu ya kujadili masoko na bei ya zao hilo kwa kile walichodai wastani wa Dola 1.65 kwa kilo inawapunja wakulima.

Na Patrick Mabula, KAHAMA.

Viongozi wa vyama vya msingi vya wakulima zao la tumbaku wa Chama kikuu cha Ushirika wilaya ya Kahama(KACU)wameilalamikia bei elekezi ya zao hilo ya Dola ya Kimarekani 1.65 kuwa ni ndogo ikilinganishwa na gharama za kilimo cha zao hilo.

Wakiongea juzi katika kikao maalumu cha kujadili masoko ya msimu wa mwaka 2021/2022 , na bei ya kuuza tumbaku, malipo ya fedha za pembejeo walisema wastani wa bei ya Dola ya 1.65 ya Kimarekani kwa kilo iliyopangwa imekuwa ni dogo ikilinganishwa na gharama za uzalishaji.

Yohana Masanja alisema wastani wa bei ya dola 1.65 iliyopangwa mwaka huu kwa makampuni kununua tumbaku yao ni ndogo na inawapunja wakulima ikilinganishwa na gharama za kilimo za mwaka huu ambapo pembejeo zilikuwa bei ya juu.

Juma Shija alisema katika msimu wa kilimo wa mwaka huu gharama za pembejeo katika kilimo cha tumbaku ikiwemo mbolea walizinunua kwa bei ya kutokana na kupanda sana kwa hiyo wastani wa bei ya kuuza wa Dola1.65 ni ndogo sana na kuomba serikali na makampuni ya ununuzi kuingalia upya.

Dionis Edward wa Tumaini Amcos ya Ulowa alisema bei ya tumbaku ipo chini sana na kuomba iongezwe ili wakulima waweze kurudisha gharama yao kwenye kilimo chao kutokana na kununua pembejeo kwa gharama ya juu tofauti na misimu iliyopita.

Wenyeviti hao na Makatibu wa Amcos za wakulima wa tumbaku wamehoji sababu inayofanya bei ya zao hilo kushuka kila mwaka kuanzia 2010 wastani wa bei ulikuwa Dola 2.06 hadi leo 2022 kuwa Dola 1.65 kwa madaraja 63 ya tumbauku wakati pembejeo na gharama za uzalishaji zimweendelea kuwa juu mwaka hadi mwaka.

Awali mwenyekiti wa KACU , Hamis Majogoro alisema ameamua kuitisha kikao hicho kwa lengo la kujadili changamoto za kilimo cha zao hilo ikiwemo masoko na bei ya tumbaku inyolalamikiwa na wakulima na anataka kuongoza ushirika huo kwa maslahi mapana ya wakulima na suala hilo ataziwasilisha serikalini.

Katibu tawala wa wilaya ya Kahama , Thimos Ndanhya kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Kahama , Festo Kiswaga alisema suala la kuwasaidia na kuwatetea wakulima na hoja hiyo ya bei haliwezi kuachiwa uongozi wa KACU pekee kwa hiyo serikali ipo pamoja nao na italifanyia kazi mala moja.
Katibu Tawala wa wilaya ya Kahama, Timoth Ndanhya alipokuwa akiongea kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Kahama, Festo Kiswaga kwenye mkutano maalumu wa chama cha ushirika KACU kilichokuwa na agenda ya kujadili masoko na bei ya tumbaku kuwa ndogo.
Mwenyekiti wa Chama kikuu cha Ushirika cha Wilaya ya Kahama (KACU ) Hamis Majogoro akiongea katika mkutano maalumu wa viongozi wa vyama vya msingi (AMCOS) vya tumbaku vya ushirika huo juu ya kujadili masoko na bei ya zao hilo kwa kile walichodai wastani wa Dola 1.65 kwa kilo inawapunja wakulima.
Viongozi wa vyama vya msingi ( AMCOS) vya zao la tumbaku Wenyeviti na Makatibu wakiwa katika kikao cha kujadili masoko ya zao hilo msimu wa 2021/2022 .
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.

Post a Comment

0 Comments