Header Ads Widget

WANANCHI WA BUPIGI WILAYANI KISHAPU WAISHUKURU SERIKALI KUWAJENGEA SHULE YA SEKONDARI

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akizungumza kwenye sherehe hizo.

Katibu wa umoja wa wazazi mkoa wa Shinyanga Regina Ndulu akizungumza kwenye sherehe hizo.

Suzy Luhende, SHINYANGA

Wananchi wa kijiji cha Wela Kata ya Bupigi wilayani kishapu, wameishukuru Serikali kwa kuwajengea shule ya Sekondari kwenye Kata hiyo ambayo ipo kwenye hatua ya kupauliwa, pamoja na barabara, na kuiomba tena iwapelekee mradi wa maji safi na salama, ambapo wamekuwa wakipata shida kufuata maji umbali mrefu.


Wamebainisha hayo jana kwenye Sherehe za Umoja wa wazazi Mkoa jumuia ya CCM Tanzania zilizofanyika kimkoa katika kijiji cha Wela kata ya Bupigi wilaya ya Kishapu.

Diwani wa Kata hiyo ya Bupigi Reuben Kisabo akiongea kwa niaba ya wananchi, amesema serikali imeendelea kuleta maendeleo mbalimbali ikiwemo barabara ya kutoka Uchunga kuelekea Bupigi, lakini kuna ya ukosefu wa maji safi na salama.

Mgeni rasimi wa sherehe hiyo ambaye alikuwa mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Mabala Mlolwa, amesema tatizo la maji linaenda kuisha, kwani tatizo la maji Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu ameshalisikia na tayari ameshatoa fedha kwa ajili ya mradi wa maji, hivyo ataliondoa muda si mrefu na watu watapata maji safi na salama ya kutoka ziwa victoria.

"Ndugu zangu Rais ameshakisikia kilio chenu tayari ameshatoa pesa kwa ajili ya mradi wa maji hivi karibuni tatizo hili linaenda kuisha kwani katoa fedha za miradi mbalimbali katika mkoa wetu ikiwemo ya kujenga madarasa hivyo hakuna mwananchi aliyechangishwa, tunatakiwa tu tujiandae kutoa ushirikiano katika zoezi zima la sensa," amesema Mlolwa.

Awali Mwenyekiti wa umoja wa wazazi jumuiya ya CCM wilaya Kishapu Gregoli Kigosi, amesema mpaka sasa wilaya ina wanachama wa jumuiya ya wazazi 8,700, ina viwanja viwili, na shule moja ya Sekondari Kanawa na matokeo ya mwaka 2022 ilikuwa ya 14 kati ya shule 128 kwenye mkoa wa Shinyanga, hivyo wameomba uzio ili kuongeza ulinzi zaidi na bwalo kwa ajili ya chakula.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa umoja wa wazazi jumuia ya CCM mkoa wa Shinyanga Salim Simba aliwaomba wananchi waendelee kujiunga na umoja wa wazazi na katika chaguzi za chama wachague viongozi wenye uwezo wa kuongoza.

Naye katibu wa umoja wa wazazi mkoa wa Shinyanga Regina Ndulu aliwashukuru sana watu waliohudhulia na walifanikisha sherehe hiyo, ambapo aliwaomba waendelee na umoja huo ikiwa ni pamoja na kudumisha amani.

Post a Comment

0 Comments