Na Marco Maduhu, NZEGA
Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu wilayani Nzega mkoani Tabora, kupitia Chama cha Wachimbaji Madini Mkoa wa Tabora (TABOREMA), wamerudisha faida kwa jamii kupitia (CSR )na kuchangia jumla ya madawati 289 na kuyakabidhi Serikalini, pamoja na kupanda miti katika Ofisi ya Kijiji cha Mwabangu.
TAZAMA VIDEO👇👇
Hafla ya kukabidhi madawati hayo imefanyika leo Mei 30, 2026, katika Kijiji cha Mwabangu kwenye Machimbo ya Isungang’wana Kata ya Nata Halmashauri ya Wilaya ya Nzega, huku mgeni rasmi akiwa Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Naitapwaki Tukai, aliyewakilishwa na Afisa Tarafa ya Puge, Rahma Mnyone.
Mwenyekiti wa TABOREMA Wilaya ya Nzega Joseph Mabondo, amesema wachimbaji wana wajibu wa kurudisha faida kwa jamii (CSR), ndiyo maana wao wameamua kuiunga mkono Serikali kwa kutoa madawati ili kuboresha sekta ya elimu.
Amesema mbali na mchango huo wa madawati, pia wamepanda miti katika Ofisi ya kijiji cha Mwabangu kama sehemu ya kuhamasisha utunzaji wa mazingira.
Naye Mgeni Rasmi Afisa Tarafa ya Puge Rahma Mnyone, amewapongeza wachimbaji hao kwa kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha sekta ya elimu kupitia mchango wa madawati, hatua ambayo amesema itasaidia kuboresha mazingira ya kujifunzia na kuongeza ufaulu wa wanafunzi.
TAZAMA PICHA👇👇
Afisa Tarafa ya Puge Rahma Mnyone akizungumza.
Mwenyekiti wa TABOREMA Wilaya ya Nzega Joseph Mabondo akizungumza.
zoezi la makabidhiano la Madawati likiendelea.
Mgeni Rasmi akipanda mti.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464