Header Ads Widget

RIPOTI YA CAG ILIVYOBAINI UPIGAJI FEDHA TAA ZA BARABARANI MALIPO YATOFAUTIANA NA MKATABA


MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) amebaini malipo ya ziada ya taa za barabarani Sh. milioni 588.45 katika Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara.


Katika ripoti yake ya ukaguzi kwa mwaka wa fedha 2020/21 iliyowasilishwa bungeni Jumanne, CAG Charles Kichere, anasema alibaini kuwa taa za barabarani zilizowekwa katika barabara mbalimbali kupitia mkataba ulioingiwa chini ya kipande Na. 5 zililipwa kwa viwango vya bei ya juu kuliko bei iliyokubaliwa kwenye mkataba.

Anasema hiyo ilichangiwa na usimamizi duni wa zabuni husika, hivyo kusababisha ongezeko la kiwango cha malipo kwa kila taa.

Ilikuwaje? CAG anafafanua kuwa kipengele cha 36.1 cha Masharti ya Jumla ya Mkataba Na. LGA/085/2017/2018/W/01 ulioingiwa tarehe 8 Juni 2018 kwa Sh. 23,176,087,870 kwa muda wa miezi 18.5 kati ya Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara na mkandarasi kinataja kuwa:

"Hati ya makisio ya gharama za ujenzi inatumika kukokotoa bei ya mkataba; na mkandarasi atalipwa kulingana na kiwango cha kazi iliyokamilika kwa bei zilizotajwa kwenye gharama za makadirio ya vifaa kwa kila kipengele."

CAG anabainisha kuwa idadi ya vitu 8,100 vilivyomo katika gharama za makadirio ya vifaa vilivyohusishwa kwenye mkataba inaonyesha kuwa...................

SOMA HAPA ZAIDI CHANZO NIPASHE.

Post a Comment

0 Comments