` STAND UNITED WAPIGWA BAO 3-1 MCHEZO WA KWANZA PLAYOFF DHIDI YA FOUNTAIN GATE

STAND UNITED WAPIGWA BAO 3-1 MCHEZO WA KWANZA PLAYOFF DHIDI YA FOUNTAIN GATE

STAND UNITED WAPIGWA BAO 3-1 MCHEZO WA KWANZA PLAYOFF DHIDI YA FOUNTAIN GATE

Na Marco Maduhu,SHINYANGA
Mechi ya Stand United na Fountain Gate imemalizika katika Uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga.

Mchezo huo ni wa Kwanza wa Playoff, ambapo mchezo wa marudiano utachezwa huko Singida Julai 8, ambapo mshindi atashiriki kucheza msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Goli la kwanza la Fountain Gate limefungwa kipindi cha kwanza na mchezaji Kasim Haroon dk 28 ,huku Stand United wakisawazisha dk ya 44 goli liliofungwa na Joram Mgeveke.

Kipindi cha pili Fountain Gate waliongeza Goli,lililofungwa na Said Sadiki dk 65.
Ambapo Goli la tatu lilifungwa na Mudrick Gonda dk 82.

Baada Goli hilo kufungwa,iliibuka vurugu na kusababisha mpira kusimama kwa muda.

Hadi dakika 90 zinamalizika Fountain Gate walibakia na Goli zao 3-1



Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464