Header Ads Widget

MWANAFUNZI AOMBA MSAADA UFADHILI WA MASOMO

MWANAFUNZI AOMBA MSAADA UFADHILI WA MASOMO

Mwanafunzi Joyce Ngassa akiomba msaada ufadhili wa masomo.
Baba Mzazi wa Joyce Ngassa, ambaye ni Ngassa Seleli akimuombea msaada wa ufadhili wa masomo Binti yake kutokana na kutokuwa na uwezo wa kumsomesha..

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MWANAFUNZI Joyce Ngassa mkazi wa kijiji cha Welezo wilayani Shinyanga, anaomba msaada wa kufadhiliwa kwenda kusoma katika Chuo cha Tarime Vocational Training College (T.V.T.C) ili akatimize ndoto zake.

Joyce Ngassa amemaliza elimu ya kidato cha Nne mwaka jana katika Shule ya Sekondari Tinde, lakini hakupata matokeo mazuri, na alipokuwa bado shuleni alijaza fomu ya kujiunga na Chuo hicho na akachaguliwa kujiunga, kutokana na wazazi wake kutokuwa na uwezo ameshindwa kwenda kuanza masomo yake na kuomba msaada wa kulipiwa Ada ili akatimize ndoto zake.

Kwa upande wa Baba yake Mzazi Ngassa Seleli, ana sema yeye hana uwezo wa kumsomesha, na watu wamekuwa wakimshawishi amuozeshe Binti yake huyo ili apate mifugo, lakini amegoma na kutaka mtoto wake asome ambapo ana imani atakuja kuwasaidia.

Anasema kwa mujibu wa fomu kutoka Chuo hicho wanapaswa kulipa Ada Sh.milioni 1.4 kwa mwaka, lakini wao hawana uwezo na kuomba wadau wajitokeze kumsaidia mtoto wake huyo ili akasome na kutimiza ndoto zake.

Kwa mtu yeyote, Mashirika, au Taasisi watakaoguswa kumsaidia Mwanafunzi huyo wawasiliane na Baba yake Mzazi Ngassa Seleli kwa simu namba. 0693225776.

Post a Comment

0 Comments