Header Ads Widget

SHIRIKA LA WEADO KUTOKOMEZA UKATILI WA KIJINSIA DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO MASENGWA WILAYANI SHINYANGA

Mkurugenzi wa Shirika la (WEADO) Mkoani Shinyanga Eliasenya Nnko, akitambulisha mradi kutokomeza matukio ya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto katika Kata ya Masengwa wilayani Shinyanga.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

SHIRIKA lisilo la kiserikali la Women Elderly Advocacy and Development Organization (WEADO) la mkoani Shinyanga, ambalo linatetea haki za Wanawake, Watoto na Wazee, limezindua mradi wa kutokomeza matukio ya ukatili kijinsia dhidi ya wanawake na watoto Kata ya Masengwa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Uzinduzi huo umefanyika leo Januari 20, 2022 kwenye Kata hiyo ya Masengwa, na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa Kata hiyo, akiwamo Diwani, Wazee Maarufu, viongozi wa dini, Baraza la watoto, Dawati la jinsia, Hakimu, Maofisa maendeleo ya jamii, na wajumbe wa Mtakuwwa.

Afisa miradi wa WEADO Salome Shangari , alisema mradi huo wa kutokomeza matukio ya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto katika Kata ya Masengwa wilayani  Shinyanga wanautekeleza kwa muda wa miezi mitatu, ambao utakoma March mwaka huu, kwa ufadhili wa mfuko wa Ruzuku wa wanawake Tanzania (WFT) wenye thamani ya Sh.milioni 12.4.

Alisema lengo la mradi huo ni kupunguza matukio ya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto, katika Kata hiyo ya Masengwa, ili jamii iishi kwa amani na utulivu bila ya kufanyiana vitendo vya ukatili.

“Kazi ambazo tutazifanya kwenye utekelezaji wa mradi huu wa kupunguza matukio ya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto katika Kata hii ya Masengwa, ni kuongeza uelewa kwa jamii kufahamu matukio ya ukatili na madhara yake, hali ambayo itasaidia kuachana na vitendo vya ukatili  wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto,”alisema Shangali.

Naye Mkurugenzi wa Shirika la WEADO Eliasenya Nnko, alisema kwa utafiti walioufanya, matukio mengi ya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto yanatokea Majumbani pamoja na Shuleni, na mengi yamekuwa yakifanywa na watu wa karibu na familia, ambapo wadau na Serikali wanapaswa kuunganisha nguvu ya pamoja kutokomeza matukio hayo.

Aidha, Mtendaji wa Kata ya Masengwa wilayani Shinyanga Hussein Majaliwa, alisema matukio ya ukatili wa kijinsia ambayo bado yapo kwenye Kata hiyo ni vipigo kwa wanawake na watoto hasa katika kipindi cha kilimo na mavuno.

Alifafanua kuwa kipindi cha kilimo wanafunzi wengi wamekuwa wakizuiwa kwenda Shule ili wakalime, na wakikataa wana ambulia kipigo, ambapo kwa upande wa wanawake kipindi cha mavuno mwanaume ndio wanauza mazao na akihoji kuhusu pesa anapata kipigo.

Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya jamii Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Joram Magana, alitaja chanzo cha matukio ya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto kuendelea kuwepo ndani ya jamii, kuwa inatokana na uendekezaji wa Mila na desturi Kandamizi.

Alitaja vyanzo vingine kuwa ni migogoro ya ndoa, wazazi kutoa vipigo kwa watoto, umaskini wa familia, tamaa ya kutaka mali kwa wazazi na kugeuza watoto wa kike vitega uchumi, pamoja na jamii kutotoa taarifa za matukio hayo, na umalizaji wa kesi kimya kimya.

Mkurugenzi wa Shirika la (WEADO) Mkoani Shinyanga Eliasenya Nnko, akitambulisha mradi kutokomeza matukio ya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto katika Kata ya Masengwa wilayani Shinyanga.
Mkurugenzi wa Shirika la (WEADO) Mkoani Shinyanga Eliasenya Nnko, akitambulisha mradi kutokomeza matukio ya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto katika Kata ya Masengwa wilayani Shinyanga.

Afisa miradi kutoka Shirika la WEADO Mkoani Shinyanga Salome Shangari, akielezea utekelezaji wa mradi wa kutokomeza matukio ya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto Kata hiyo ya Masengwa wilayani Shinyanga.

Afisa Tathimini na ufuatiliaji kutoka Shirika hilo la WEADO John Eddy, akizungumza kwenye uzinduzi wa mradi huo.

Diwani wa Masengwa Nicodemas Simon, akizungumza kwenye uzinduzi wa mradi huo.

Afisa Maendeleo ya jamii wilaya ya Shinyanga Joram Magina, akizungumza kwenye uzinduzi wa mradi huo.

Mtendaji wa Kata ya Masengwa Husseni Majaliwa akizungumza kwenye uzinduzi wa mradi huo.

Mkuu wa Dawati la Jinsia Polisi wilaya ya Shinyanga Brightone Rutajama,akizungumza kwenye uzinduzi wa mradi huo.

Mkuu wa Dawati la Jinsia Polisi wilaya ya Shinyanga Brightone Rutajama,akizungumza kwenye uzinduzi wa mradi huo.

Wajumbe wakiwa kwenye uzinduzi wa mradi wa kutokomeza matukio ya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto katika Kata ya Masengwa wilayani Shinyanga.

Uzinduzi wa mradi ukiendelea.

Uzinduzi wa mradi ukiendelea.

Uzinduzi wa mradi ukiendelea.

Uzinduzi wa mradi ukiendelea.

Uzinduzi wa mradi ukiendelea.

Uzinduzi wa mradi ukiendelea.

Uzinduzi wa mradi ukiendelea.

Uzinduzi wa mradi ukiendelea.

Picha ya pamoja ikipigwa mara baada ya kumalizika uzinduzi wa mradi wa kutomeza ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto katika Kaya ya Masengwa wilayani Shinyanga.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA.
TUTUMIE HABARI,PICHA,MATUKIO AU TANGAZO LAKO TUKUWEKEE KWENYE SHINYANGA PRESS CLUB BLOG,WASILIANA NASI KWA Email : shinyapress@gmail.com Simu/WhatsApp 0756472807