Header Ads Widget

DK TULIA APITISHWA KUWA MGOMBEA PEKEE NAFASI YA SPIKA

                              Dk. Tulia Akson 


Kamati kuu ya halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi(CCM) imepitisha jina la Dk.Tulia Akson kuwa mgombea kiti cha spika nafasi ambayo iliachwa wazi na Job Ndugai baada ya kujiuzulu mapema mwezi huu.

Katibu Mwenezi wa CCM Shaka Hamdu Shaka ametoa taarifa hiyo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa White House Jijini Dodoma na kueleza kuwa kamati kuu imepitisha jina pekee la Dk. Tulia Akson kati ya majina 70 ya wanaCCM waliochukuwa fomu na kurejesha.
TUTUMIE HABARI,PICHA,MATUKIO AU TANGAZO LAKO TUKUWEKEE KWENYE SHINYANGA PRESS CLUB BLOG,WASILIANA NASI KWA Email : shinyapress@gmail.com Simu/WhatsApp 0756472807