Header Ads Widget

WALENGWA TASAF WAELEZA UFUGAJI KUKU NAMNA ULIVYOWAKOMBOA KWENYE UMASKINI

Mlengwa wa TASAF Makubi Luhangija, akiwa na Maofisa wa TASAF, akieleza namna fedha za TASAF zilivyompatia unafuu wa maisha, ambapo alianza kununua kuku, kisha kiwanja akajenga nyumba na kuezeka bati.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

WALENGWA wa mpango wa kunusuru Kaya Maskini TASAF katika vijiji vya Buduhe na Nzonza wilayani Shinyanga, wameeleza namna walivyozitumia fedha za TASAF kununua kuku na kuwapatia mafanikio mengi ikiwamo kujenga nyumba na kuezeka bati.

Wamebainisha hayo leo kwa nyakati tofauti, wakati Maofisa wa TASAF Mkoa wa Shinyanga, walipofanya ziara ya kukutana na walengwa hao, kuelezea mafanikio ambayo wameyapata kupitia fedha za TASAF, pamoja na changamoto ambazo zinawakabili kwenye mpango huo ili zitafutiwe ufumbuzi.

Miongoni mwa walengwa hao Makubi Luhangija mkazi wa kijiji cha Buduhe, alisema mara baada ya kuanza kupokea fedha hizo za TASAF, alianza na ufugaji wa kuku ambao waliongezeka na kufikisha 70, ambapo aliwauza na kununua kiwanja, huku akiendelea na ufugaji huo wa kuku hadi akajenga nyumba na kuezeka bati.

Mlengwa mwingine wa TASAF Neema Dalali Mkazi wa kijiji cha Nzonza, alisema yeye alianza na ufugaji huo wa kuku, ambao aliwauza na kununua Mbuzi watatu, na sasa amenunua Mabati 10 ambayo ataezeka kwenye nyumba yake aliyoijenga kupitia fedha hizo za TASAF.

"Tunaishukuru sana Serikali kwa kutoa fedha hizi za TASAF ambao zimetusaidia kutuondoa kwenye hali mbaya ya umaskini na kupata unafuu wa maisha," walisema walengwa hao kwa nyakati tofauti.

"Changamoto kubwa ambayo inatukabili kwa sasa kwenye ufugaji huu wa kuku ni magonjwa, kuku wanakufa sana hali ambayo tunahofia kurudi tena kwenye umaskini wa kupindukia," alisema Mariam Athanasi.

Pia, walisema changamoto nyingine ambayo inawakabili ni suala malipo kwa njia ya simu, ambapo baadhi yao hawana simu na wala wajui kusoma, na kuomba waendelee kulipwa kwa mfumo wa kawaida.

Naye Mratibu wa TASAF Mkoa wa Shinyanga Dotto Maligisa, aliwataka maofisa mifugo wote mkoani humo, watoe elimu ya ufugaji bora wa kuku kwa walengwa wa TASAF, pamoja na kuwapatia chanjo ili kuku wao wasife na magonjwa.

Aidha, alisema kwa wale walengwa ambao bado wanakabiliwa na chagamoto ya malipo kwa mfumo wa simu, wataendelea kulipwa pesa zao kwa njia ya kawaida.

Kwa upande wake Afisa ufuatiliaji wa TASAF Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na Manispaa ya Shinyanga Tabu Maro, alitoa wito kwa walengwa hao kuwa fedha ambazo wanazipata wasizumie vizuri ili ziwatoe kwenye umaskini.

Katika hatua nyingine, aliwataka wajiunge kwenye mfuko wa bima ya Afya CHF, ambao utawarahisishia kupata matibabu bure na kuokoa Afya zao, sababu magonjwa haya hodi.

Katibu Tawala Msaidizi uchumi na uzalishaji mkoani Shinyanga Beda Chamatata, aliwataka walengwa hao kuwa katika fedha hizo, licha kuwekeza kwenye shughuli za uzalishaji pia wawapeleke watoto shule na kliniki.

Mratibu wa TASAF Mkoa wa Shinyanga Dotto Maligisa, akizungumza na walengwa wa TASAF kutoka katika vijiji viwili vya Buduhe na Nzonza Kata ya Salawe wilayani Shinyanga.

Mratibu wa TASAF mkoani Shinyanga Dotto Maligisa, akisiliza changamoto za walengwa wa TASAF na kuzitafutia ufumbuzi.

Afisa ufuatiliaji wa TASAF Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na Manispaa ya Shinyanga Tabu Maro, akizungumza na walengwa wa TASAF.

Katibu Tawala Msaidizi uchumi na uzalishaji mkoani Shinyanga Beda Chamatata, akizungumza na walengwa wa TASAF.

Walengwa wa TASAF wakiwa kwenye mkutano wa viongozi wa TASAF wa kueleza mafaniko na changamoto ambazo zinawakabili.

Walengwa wa TASAF wakiwa kwenye mkutano wa viongozi wa TASAF wa kueleza mafaniko na changamoto ambazo zinawakabili.
Mlegwa wa TASAF Neema Dalali akielezea mafanikoo ambayo ameyapata kupitia fedha za TASAF, ambapo alianza na ufugaji wa kuku lakini sasa ana Mbuzi watatu na Bati 10 kwa ajili ya kuezeka kwenye nyumba yake na kutoishi tena kwenye nyumba ya Nyasi.

Mlengwa wa TASAF Suzana Shija, akieleza mafanikio ambayo ameyapata kupitia fedha za TASAF kuwa ana Mbuzi Wanne na amejenga nyumba ya Bati.

Mlengwa wa TASAF Justina Malale, akielezea mafanikio ambayo ameyapata kupitia TASAF, kuwa amenunua kiwanja, pamoja na Bati 10 kwa ajili ya kuezeka kwenye nyumba yake.

Mlengwa wa TASAF Tatu Bukwimba, akielezea mafanikio ambayo ameyapata kupitia fedha za TASAF ambapo alianza na ufugaji wa kuku. lakini sasa ana Hekali Tatu za Shamba, pamoja na Kondoo Nane.

Mlengwa wa TASAF Helena Makoye, akielezea mafaniko ambayo ameyapata kupitia fedha za TASAF kuwa alianza na ufugaji wa kuku, lakini sasa ana Kondoo Nane, Bati 10 ambazo anatarajia kuezeka kwenye nyumba yake, aliyojenga kupitia fedha za TASAF.

Mlengwa wa TASAF Makubi Luhangija, akiwa na maofisa wa TASAF, akieleza namna fedha za TASAF zilivyompatia unafuu wa maisha, ambapo alinunua kiwanja na kisha kujenga nyumba na kuezeka bati na kutoka kwenye Nyasi.
 
Na Marco Maduhu, SHINYANGA.

Post a Comment

0 Comments