Header Ads Widget

KAMATI YA SIASA YA CCM SHINYANGA,YATAKA UKAMILISHAJI MAJENGO KITUO CHA AFYA SALAWE

 

 Mwonekano wa jengo la ujenzi  la kituo cha afya Salawe katika ziara ya Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga Alhamisi 27,januari,2022.

Wajumbe wa Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga wakikagua ujenzi wa jengo la kituo cha afya salawe Alhamisi 27,januari,2022.
 
Na Kareny  Masasy.
 
Kamati ya siasa ya  Chama Cha Mapinduzi(CCM)  Mkoa wa Shinyanga  haijaridhishwa na kasi ya ujenzi wa majengo ya upasuaji,mochwari na wodi ya mama na mtoto  kituo cha afya Salawe  katika Halmashuri ya wilaya ya Shinyanga licha ya serikali kutoa kiasi cha fedha Shs milioni 250 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya.

Hayo yamelezwa,Janauri 27,2022  wakati ziara ya Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi ya Mkoa wa Shinyanga,ikiongozwa  na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Bw,Mabala Mlolwa.Kamati hiyo ilieleza kuwa hajaridhishwa na hatua za ujenzi wa kituo hicho kulingana na maeneo mengine kuwa yamekwisha kamilisha ujenzi wa vituo vya afya.

Kamati ya Siasa ya CCM ilieleza kuwa hali ya ucheleweshaji wa ujenzi wa kituo cha afya cha Salawe unatokana na kamati ya afya ya kituo hicho kukwamisha juhudi za haraka za ujenzi huo kwa ajili ya manufaa ya wananachi wa kata ya Salawe.

Kamati hiyo ya CCM ilitoa maagizo kwa kamati ya afya kuchukua hatua za haraka za ukamilishaji wa ujenzi wa kituo cha afya salawe kwa ajili ya kutoa huduma za afya kwa wakazi wa salawe.

Aidha,Mary Shausi ambaye ni  Mtendaji wa kata ya Salawe  akitoa taarifa mbele ya wajumbe wa kamati hiyo amesema kuwa   walipokea kiasi cha fedha kwa ajili ya mradi huo  ila wanatarajia kukamilisha ifikapo mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu.


Post a Comment

0 Comments