Header Ads Widget

SHIRIKA LA GCI LAENDESHA MAFUNZO YA STADI ZA MALEZI NA MAKUZI YA MTOTO KUPINGA VITENDO VYA UKATILI KATA YA PUNI NA NYIDA WILAYANI SHINYANGA

Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Christopher Malengo, akitoa mafunzo ya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto kwa wananchi wa Kata ya Puni na Nyida wilayani humo.

Na Shaban Njia, SHINYANGA.

SHIRIKA lisilo la kiserikali la Green Community Inititives(GCI) limeendesha mafunzo ya Mafunzo ya Stadi za malezi na makuzi ya mtoto ili kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto, kwa wananchi wa kata za Puni na Nyida Wilayani Shinyanga.

Mafunzo yaliyotolewa ni elimu juu ya malezi ya familia, Mazingira salama ya mtoto, vyanzo vya ukatili, aina za ukatili wa kijinsia, Mbinu wezeshaji za watoto kujilinda, Mazingira salama ya watoto wenye ulemavu, vyanzo vya migogoro pamoja na elimu ya kuimarisha uchumi wa kaya.


Utoaji wa mafunzo hayo ni utekelezaji wa mradi wa “TUWALINDE” unaotekelezwa katika kata za Puni na Nyida Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kwa ufadhiri wa Mfuko wa Wanawake Tanzania(WFT) na ulianza tangu junuari mwaka huu na unatarajia kufika kikomo mwezi machi.


Akiendesha mafunzo hayo leo tarehe 28/01/2022 Ofisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Christopher Malengo amesema,moja ya sababu inayosababisha kuwepo kwa vitendo vya kikatili ndani ya familia ni kutokuwepo kwa maelewano baina ya mama na baba hali ambayo baba anafanya vitendo vya maamzi bila kushirikisha familia nzima.


Amesema, asilimia 60 ya ukatili wa kijinsia unafanywa ndani ya familia na wanafamilia kushindwa kutoa taarifa katika vyombo vya ulinzi na usalama kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria kwa kutishwa kutengwa na familia na wengi wamekuwa wakiendelea kuumia kwa kukambatia maovu.


“Watoto wengi wanafanyiwa vitendo vya kikatili na wazazi wao ama wanafamilia lakini wanashindwa kuyaripoti kwa kutishwa kupigwa au kutengwa na familia,na hii inatokana na malezi mabaya aliyopewa na wazazi wao na ndio maana wanapokuwa na kujitegeema nao wanaendekeza matukio hayo”Amesema Malengo.


Aidha amewataka wazazi na walezi kuachana na mila potofu ambayo inamkandamiza mtoto na kumnyima uhuru wa kusoma na kutoa ushauri ama maazi ndani ya familia badala yake wahakikishe wanawasimamia katika masomo yao na kumaliza salama ili waje kuwa mkombozi kwa familia zao hapo baadae.


Pia aliwataka kujiunga katika vikundi vya ujasiriamali vilivyopo katika kata na vijiji zao ili kuhakikisha wanakuwa na shughuli ya kufanya ya kujiingiza kipato ndani ya familia kwa kuwashirikisha waume zao kwa sababu mikopo isiyokuwa na riba inayotolewa na Halamshauri ipo kwa ajili yao.


Naye Meneja mradi wa Shirika la Green Community Inititives(GCI) George Nyanda, amesema mradi huo utawafikia na kuwapatia elimu ya ukatili wa kijinsia wazazi 500, kati ya hao wanawake  watakuwa 200 na wanaume 300 lengo likiwa ni kupunguza matuko hayo ndani ya jamii.

Amesema, wanaume watawatembelea katika vijiwe mbalimbali ikiwemo vya kahawa na baa na kuwapatia elimu ya stand za malezi na makuzi kwa watoto, ukatili wa kijinsia na vyanzo vyake nakwamba itasaidia kuwafungua upeo,kutoa ushirikiano na kuyaripotiwa matukio ya ukatili pale yatakapokuwa yanajitokeza kwenye jamii.

Pia Nyanda amesema kuwa,wataunda mabaraza sita ya watoto ngazi za vijiji na mabaraza mawili ngazi ya kata lengo likiwa ni kuwawezesha watoto kutambua hali zao pamoja na kutambua wapi wataweza kupata haki zao pale watakapofanyiwa vitendo vya kikatili.

Kwa upande wake,Ofisa mtendaji wa kata ya Puni Fumbuka Mathias wameingia makubaliano na wananchi wa vijiji vitatu vya kata hiyo kuwasindikiza watoto wao katika maeneo ya minada na magulio ili kuwalinda dhidi ya wanaume ambao wanaweza kuwafanyia vitendo vya kikatili ikiwemo ubakaji na ulawiti.


Amesema,lengo la kuweka makubaliano hayo ni kuhakikisha mtoto wa kike anasoma na kuhitimu masomo yake katika hali ya usalama kwani wamebaini siku za magulio na minada ndipo yanapokwenda kufanyika matendo maovu dhidi ya watoto wao na kusababisha kukatisha masomo yao.

Kadhalika wamepitisha sheria ndogo za vijiji,hakuna ndoa yoyote itakayofungwa katika vijiji vyao bila uongozi wa serikali za vijiji na Ofisi ya mtendaji wa kata kufahamu ili kujiridhisha kuwa mtu anayekwenda kufunga ndoa anaumri ambao unahitajika nasio kuoa watoto wadogo chini ya miaka 18.


Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo Happynes Shabani amesema, kwa elimu aliyoipata juu ya umuhimu wa elimu atahakikisha watoto wake wote wanasoma katika hali ya usalama na atawahamasisha majirani zake kuwapeleka shule na kuchana na tabia ya kuwakandamiza watoto.

Nae Angelina Mathias kutoka kata ya Nyida amesema,amejifunza namna ya kushirikisha familia katika maamzi ya pamoja hasa kwa kushirikisha watoto kutoa maamzi yao,malezi yanayozingatia usalama wa mtoto, watoto kwenda shule na kuwakatia vyeti za kuzaliwa.
Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Christopher Malengo, akitoa mafunzo ya ukatili kwa wananchi dhidi ya wanawake na watoto.
Baaadhi ya wananchi wa kata ya Puni na Nyida wakiendelea kupatiwa mafunzo ya kutokomeza ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto ili wakawe mabalozi wazuri kwa wenzao kutokomeza matukio hayo.

Na Shabani Njia, SHINYANGA.

Post a Comment

0 Comments