Header Ads Widget

AOMBA MSAADA KUMPATIA MATIBABU MTOTO WAKE, MUME AMKIMBIA NA KUMTELEKEZEA MTOTO

Salome Mwashitete akiwa na mtoto wake mwenye tatizo la ulemavu wa viungo.

Na Suzy Butondo, SHINYANGA

Salome Mwashitete mwenye umri wa (43) mkazi wa Kata ya Ndembezi manispaa ya Shinyanga, mwenye mtoto ambaye anatatizo la ulemavu wa viungo, amewaomba watanzania na wasamalia wema, wamsaidie fedha ili aweze kumpeleka mtoto wake hospitali kwa ajili ya matibabu zaidi, kwani mme wake alimkimbia na kumtelekezea mtoto, baada ya kuona anatatizo la ulemavu.

Ombi hilo amelitoa baada ya kutembelewa nyumbani kwake SHINYANGAPRESS Blog, ambapo amewaomba watanzania wamsaidie fedha ya kulipia matibabu ya mtoto wake mwenye ulemavu ili aweze kumpeleka hospitali kwa ajili ya matibabu na kuweza kunyoshwa baadhi ya viungo vya mwili wake angalau aweze kutembea.


Salome alisema mwaka 2007 alijifungua mtoto wa kike ambaye alianza kushituka shituka baada ya wiki moja, alipompeleka hospitali ya Muhimbili alipimwa akaonekana kwenye kichwa kuna sehemu ipo wazi, ambapo kwa sasa mtoto huyo ana umri wa miaka 14, licha ya kutembelea hospitali mbalimba lakini tatizo la mtoto wake halijapata ufumbuzi.


"Baada ya kuonekana hivyo alianza kutibiwa, lakini baada ya muda alibadilika akaanza kushituka na kuanguka kama kifafa, daktari aliyekuwa akimtibu alisema hali hiyo inasababishwa na tatizo la kichwa katika sehemu zenye uwazi, hivyo mpaka Sasa mtoto huyo hawezi kutembea anaweza kukaa tu kusimama mwenyewe hawezi lakini anaamini akipata watu wakumsaidia anaweza kutembea kidogo"alisema Salome.


Aidha Salome alisema awali mtoto huyo alikuwa akitibiwa bure, lakini kwa sasa ukienda hospitali hutibiwa bure unatakiwa ulipe Sh 5000 ndiyo umuone daktari na ukitoka hapo ukanunue dawa, pia alikuwa akifanyiwa mazoezi ili angalau aweze kutembea lakinini uwezo tena hana,na mtoto huyo anatakiwa kutumia kila siku dawa ambayo ananunua Sh 5000.

"Kama unavyomuona mtoto huyu ni wa kulisha anajisaidia hapo hapo, hivyo anatakiwa kuvaa pempas lakini Sina uwezo mme wangu baada ya kumuona mtoto haponi amekuwa mlemavu alinikimbia nikiwa nimelazwa hospitali akaenda kuowa mwanamke mwingine akaniacha nahangaika na mtoto wangu tulishakata bima ya afya lakini ukienda hospitali ya rufaa ya mkoa bima haitumiki"alisema Salome.


"Mimi ni fundi cherehani mzuri nilikuwa na cherehani yangu baada ya mtoto wangu kuugua tena niliiuza ili aweze kipatiwa matibabu, hivyo kwa sasa sina hela ya kunisaidia sina pa kushika nimekuwa mtu wa kulia kila siku,hivi karibuni mtoto aliugua nikampeleka hospitali nikaambiwa kuwa anautapia mlo nikashauriwa nimpe chakula chenye lishe lakini sina uwezo wa kupata chakula hicho kwa sababu sina pa kushika"


"Nawaomba watanzania wenzangu mashirika mbalimbali mnisaidie angalau nipate fedha ya kununua Cherehani na mtaji ili niweze kumlea vizuri kwani siwezi kumuacha peke yake ndani anahitaji kusaidiwa mara kwa mara nikiwezeshwa naweza, wengine walishasema kuwa mtoto anafungiwa ndani wakati mwingine unamuacha ndani ili tu niende nikamtafutie chochote, nisaidieni jamani namba yangu ni 0785565612 "alisema Salome.


Baadhi ya majirani wanaoishi karibu na Salome, Sophia Shija alisema kwa kweli mama huyo anatakiwa asaidiwe kwani hana uwezo hapo alipo anaishi kwa mama yake na mama yake ni mzee hana uwezo wa kumsaidia ni vizuri watanzania na sekta mbalimbali zikajitokeza kumsaidia huyu mama mtoto anahitaji lishe lakini uwezo hana, mtoto anaugua mara kwa mara lakini hana fedha ya kununulia hata dawa.


Afisa maendeleo ya jamii kata ya Ndembezi Jackson Njau alisema kweli mama mwenye mtoto mwenye ulemavu wanamfahamu vizuri na wameshawahi kumtafutia wadau wa kumsaidia wakaahidi kumsaidia, lakini mpaka sasa bado hajasaidiwa chochote kweli anapata shida sana kwani mtoto ana miaka 14 lakini ukimuona utafikiri ni mtoto wa miaka saba.


"Tunawaomba wadau mbalimbali wajitokeze ili aweze kusaidiwa huyu mtoto, huu ni mwaka wa tano sasa namhangaikia apate msaada angalau mtoto aweze kupata nguvu na kwenda shule, wajitokeze hata watu wenye mashirika wanaosaidia watoto Kama hawa wamsaidie huyu mama anashida sana kwa kweli"alisema Njau.

Post a Comment

0 Comments