Header Ads Widget

WAZAZI WAHAKIKISHE USALAMA NA ULINZI WA WATOTO KIPINDI CHA SIKUKUU.

 

 

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando

 Na Mwandishi wetu.

Wazazi na walezi wa mkoa wa Shinyanga wameaswa kuwa walinzi kwa watoto wao katika kusherekea sikukuu za krismasi na mwaka mpya, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP -George Kyando amesema hayo leo Alhamisi 23, Desemba,2021 wakati wa Mkutano wake na Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga katika salaam za Jeshi la Polisi kwa wakazi wa mkoa wa Shinyanga juu ya kipindi cha sikukuu za krismasi na mwaka mpya.

Kamanda Kyando alitaka wazazi na walezi wa watoto kuwa umakini katika kusherekea sikukuu za krismasi na mwaka mpya kwa kuangalia usalama na ulinzi wa watoto wao ili kuepuka matukio yenye kuleta athari kwa maisha ya watoto katika kipindi hiki cha sikukuu za krismasi na mwaka mpya.

Kamanda Kyando alisema wazazi na walezi wamekuwa na tabia ya kuwaacha watoto wao majumbani pekee yao bila watu wazima na kwenda katika ibada na starehe za jioni bila ungalizi wa mtu mzima majumbani, kitu ambacho wahalifu wanapata nafasi ya kuiba na kudhuru watoto.

Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga limepiga marufuku juu ya disco toto na hakuna mtu yeyote atakaye fanya shughuli zinazohusiana na disco toto kwa kipindi cha sikukuu hizi za krismasi na mwaka mpya kwa mkoa wa Shinyanga.

 Jeshi la polisi halijapokea kibali cha mtu yeyote atakayefanya shughuli ya kuendesha disco toto kwa mkoa wa Shinyanga na pia nawataka wazazi na walezi kuwa makini kulinda watoto wao katika kusherekea sikukuu za krismasi na mwaka mpya kwa kutowaacha majumbani pekee yao na pia wahakikishe watoto wanacheza maeneo ya wazi yenye usalama”

Shinyanga Press Club blog iliingia mitaani na kuzungumzia na wakazi wa manispaa ya Shinyanga kutaka kujua wamepokea vipi agizo la jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga, Halima Mussa (32) mkazi wa miti mrefu, Manispaa ya Shinyanga alisema kuwa, Kauli ya jeshi la polisi ni sahihi kwa kuwa hali ya maadili kwa jamii imepungua na hakuna mtu anayelinda mtoto wa mtu zaidi ya mhusika mwenye kuwa makini na watoto wake kwa nyakati hizi.

Evarist Kabaro, mkazi wa Ndembezi alisema, anapongeza tamko hilo la polisi kwa kuwa linaepusha vishawishi vya ngono kwa watoto kutoka kwa watu wenye tabiia chafu za kuwataka watoto kimapenzi na kuleta athari mbaya kwa watoto na gharama kwa wazazi.

 MWISHO

 

Post a Comment

0 Comments