Header Ads Widget

MWANAUME AMUUA MKEWAKE KWA KUMKATA MAPANGA NYUMBANI KWA BALOZI, NA KISHA KUJISALIMISHA POLISI , WIVU WA KIMAPENZI


Picha ya Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga George Kyando, aliyetoa Taarifa kwa waandishi wa habari juu ya tukio la mauaji.


Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MWANAMKE ambaye ni mkazi wa Mtaa wa Mbulu Kata ya Mhongolo Halmashauri ya Manispaa ya Kahama Regina Jiyenze(45) amedaiwa kuuawa na mumewake Heneriko John(53) kwa kumkata mapanga kichwani na mabegani, kisha kujisalimisha kwa jeshi la Polisi.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyang George Kyando , akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo, amesema tukio hilo limetokea leo majira ya saa Tatu asubuhi, katika Mtaa wa Mbulu Kata ya Mhongolo Manispaa ya Kahama.

Amesema chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi, ambapo mtuhumiwa alikuwa akimtuhumu marehemu kuwa sio mwaminifu kwenye ndoa yao, kitendo ambacho kilimfanya mtuhumiwa kujichukulia sheria mkononi na kumkata mapanga na kusababisha mauaji.

“Eneo la tukio tumeokota panga lenye damu likiwa umbali wa mita 20 kutoka katika eneo la tukio lilipotendeka, mtuhumiwa tunamshikilia mara baada ya kujisalimisha mwenyewe, na tutamfikisha mahakamani baada ya upelelezi kukamilika,”alisema Kyando.

“Mbinu iliyotumika ya kumkata mapanga mkewake ni kumvizia Marehemu, wakati akiwa nyumbani kwa balozi Manungu Bundala, alipofika kwa ajili ya kushitaki kutishiwa kuuawa na mumewake, ndipo alipokatwa mapanga sehemu za kichwani na mabengani na kufariki dunia,”aliongeza.

Pia Kamanda alitoa wito kwa wananchi kujiepusha na vitendo vya kujichukulia sheria mkononi, kisa wivu wa mapenzi, kwani kitendo hicho hakifai na kinaonekana kimekuwa sugu, huku akitoa ushauri kwa wapenzi au wanandoa ,kuwa wakiona  mwenzake sio mwaminifu kwenye mahusiano waachane, ambapo wataingia kwenye matatizo kujutuia kwenye maisha yao.
 
Na Marco Maduhu- SHINYANGA.
 

Post a Comment

0 Comments