Header Ads Widget

SHUHUDIA GARI LILIVYO TUMBUKIA BAHARINI POLISI WATIA NENO Dar es Salaam. Gari aina ya Toyota Landcruiser Prado limetumbukia katika Bahari ya Hindi eneo la ufukwe wa Coco huku polisi wakieleza kusubiri afya ya dereva wa gari hilo kuimarika ili waanze uchunguzi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi Kinondoni, Ramadhani Kingai ameieleza Mwananchi Digital leo Jumanne Oktoba 5,2021 kuwa hakuna madhara yoyote yaliyotokana na ajali hiyo baada ya mtu huyo kuokolewa.

Amesema wanasubiri afya yake iimarike ili wafanye uchunguzi wa tukio hilo kwa kuwa dalili zinaonyesha alikuwa ni mtu mwenye mawazo au tatizo la akili.


"Kule alipokuwa anakwenda kulikuwa hakuna barabara, kama mtu ni mzima huwezi kuona gari linakwenda baharini na wewe ukazidi kukanyaga mafuta," amesema Kingai.

             SOMA ZAIDI HAPA ;CHANZO MWANANCHI

 

 

 

Post a Comment

0 Comments