Header Ads Widget

MKURUGENZI SHIRIKA LA TVMC AWAFUNDA WANAFUNZI SHULE YA SEKONDARI DON BOSCO


Musa Ngangala Mkurugenzi Shirika TVMC na Mjumbe NACONGO, akizunguma na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Don Bosco.


Na; Josephine Charles, SHINYANGA.

 
MKURUGENZI wa Shirika la The Voice of Marginalized Community(TVMC) bw. Musa Ngangala ambaye pia ni  Mjumbe wa baraza la Taifa la National Council of Non Government Organization (NACONGO) Mkoa wa Shinyanga,  amewaasa wanafunzi wa shule ya Sekondari Don Bosco iliyopo Didia mkoani Shinyanga, waishi katika ukweli na uwazi, kama alivyosisitiza Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere enzi za uhai wake.

Ameyasema hayo katika mdahalo maalum ulioandaliwa na shule hiyo uliokuwa na lengo la kukumbusha,kuelimisha pamoja na kuyaenzi maisha ya aliyekuwa Rais wa kwanza Tanzania na baba wa taifa hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere kwa wanafunzi hao hasa kufanya tathmini ya kupingwa kwa wale maadui watatu ambao ni Ujinga,Maradhi na Umaskini enzi za uhai wake ilikuwaje na baada ya kufariki ikawaje pamoja na nini kifanyike ili kuendelea kupinga maadui hao.

Bwana Ngangala ameeleza namna ambavyo hayati baba wa taifa mwl. Nyerere alikuwa akiilinda Tanzania kwa fikra zake thabiti zenye manufaa ambapo alikemea ubaguzi wa rangi,ukabila,ufisadi,Uzalimu na wizi ndiyo maana akawa muumini wa kuanzishwa kwa mahakama za ufisadi pamoja na kuanzisha tume mbalimbali za haki za bianadamu.

Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wakiwemo Josephine Teshasha na Mabula Maganga kupitia mdahalo huo wamesema ili kuweza kuendelea kupinga maadui watatau ambao ni Ujinga,Maradhi na Umaskini ni vyema serikali ikaendelea kuwekeza nguvu kutoa Elimu za kuzuia Ukatili wa kijinsia kwa watoto kwa sababu bila kufanya hivyo maadui hao wataendelea kuwazunguka na kusababisha maendeleo hafifu hasa katika sekta ya Elimu Tanzania.

Naye Mkuu wa Shule hiyo Padre Felix Wagi amesema mdahalo huo umewajengea umahiri wanafunzi wao na kuwakumbusha maadui watatu ambao ni Ujinga,Maradhi na Umaskini na ameahidi katika shule yao wataendelea kuyaenzi yale mazuri aliyoyafanya Mwl. Nyerere enzi za uhai wake kwa vitendo.

Wanafunzi wa Don Bosco wakiwa ukumbini wakisikiliza nasaha.
Wanafunzi wa Don Bosco wakiwa ukumbini wakisikiliza nasaha.

Wanafunzi wa Don Bosco wakiwa ukumbini wakisikiliza nasaha.































Post a Comment

0 Comments