Header Ads Widget

KATAMBI AFANYA ZIARA UKAGUZI UJENZI MADARAJA, AONYA WAKANDARASI WATAKAOTEKELEZA MIRADI CHINI YA KIWANGO.


Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, na Ajira, (kulia) akikagua ujenzi wa Daraja la Bugwandege- Uzogole, katikati ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abubakari Mukadamu, kushoto ni Kaimu Meneja Wakala wa Barabara Mjini (TARURA) Manispaa ya Shinyanga Mhandisi Yohana Marwa.


Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MBUNGE wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, amefanya ziara ya kukagua ujenzi wa Madaraja mjini humo, na kuwaonya  Wakandarasi ambao watatekeleza miradi chini ya kiwango.
 
Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira, amebainisha hayo leo wakati alipomaliza kufanya ziara ya kukagua ujenzi wa madaraja ya Uzogole- Bugwandege, Iwelyangula, na Upongoji la watembea kwa miguu.

Alisema Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi, hivyo kwa Wakandarasi ambao wanapewa kazi mjini Shinyanga, wajipange kisawasawa kutekeleza miradi hiyo kwa kiwango cha juu kulingana na thamani ya fedha (Value for Money).

"Nimekagua ujenzi wa Madaraja Matatu, ambapo nimeona utekelezaji wake, na jingine limeanza kufanya kazi la Iwelyangula, ila naonya Wakandarasi ambao watavurunda kazi zao, hawatapata kazi tena hapa Shinyanga," alisema Katambi.

"Mfano katika daraja hili la Uzogole- Bugwandege limegharimu Sh.milioni 190, Iwelyangula Sh. milioni 428, na daraja la Upongoji la watembea kwa miguu Sh.milioni 100, ni fedha nyingi na sitakubali zichezewe," aliongeza.

Katika hatua nyingine, alisema Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassani, imeendelea kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha changalawe, ambapo kwa Shinyanga itapewa jumla ya Sh.bilioni 1.5.

Pia, alisema Serikali imeshatoa Sh.milioni 250 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya Oldshinyanga ,pamoja na Sh.milioni 700, kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya Madarasa kwa shule za Sekondari Manispaa ya Shinyanga.

Aidha, alisema Serikali itapeleka pia vifaa tiba katika kituo cha Afya Kambarage vikiwamo vipimo vya MRA, pamoja na X-RAY, kwa ajili ya kuboresha huduma za matibabu kwa wananchi.

Naye Mwenyekiti wa jumuiya ya wanawake wa Chama Cha Mapinduzi CCM (UWT) Lucy Enock, akizungumza kwa niaba ya Katibu wa Chama hicho Agnes Bashemu, alimpongeza Mbunge Katambi kwa kutekeleza ilani ya chama kwa vitendo.

Nao baadhi ya wananchi, na wanafunzi ambao wamejengewa Madaraja hayo, akiwamo Mwanafunzi Vailet Adamu, walishukuru ujenzi wake, hasa daraja la Iwelyangula, ambapo la zamani lilisombwa na maji, na hivyo kipindi cha Masika walikuwa wanashindwa kwenda shule.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, na Ajira, (kulia) akikagua ujenzi wa Daraja la Bugwandege- Uzogole, katikati ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abubakari Mukadamu, kushoto ni Kaimu Meneja Wakala wa Barabara Mjini (TARURA) Manispaa ya Shinyanga Mhandisi Yohana Marwa.

Katambi akiangalia maendeleo ya ujenzi wa daraja la Uzogole- Bugwandege.

Katambi akiangalia maendeleo ya ujenzi wa daraja la Uzogole- Bugwandege.

Maendeleo ya ujenzi wa Kingo katika daraja la Bugwandege- Uzogole ukiendelea.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, na Ajira, wapili kulia, akiangalia ujenzi wa daraja la Iwelyangula ambalo linaunganisha Kata ya Chamaguha na Kitangili.

Muonekano wa daraja jipya la Iwelyangula.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, na Ajira, akizungumza na wanafunzi kuelezea adha ambayo waliipata mara baada ya daraja la awali kusombwa na maji.

Muonekano wa daraja la zamani la Iwelyangula ambalo limekatika mara baada ya kusombwa na maji.

Muonekano wa ujenzi wa daraja la Upongoji la watembea kwa miguu.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, na Ajira ,(mwenye suti katikati), akipiga picha ya pamoja na viongozi wa Chama (CCM), Pamoja na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, (katikati mwenye suruali), alipofika kuzungumza na Mkuu huyo wa wilaya kabla ya kuanza ziara yake ya ukaguzi wa ujenzi wa Madaraja.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA.


Post a Comment

0 Comments