Header Ads Widget

MKURUGENZI MANISPAA YA SHINYANGA ATANGAZA NEEMA KWA WANAFUNZI SHULE ZA MWAMALILI, MWAWAZA NA KIZUMBI



Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura akizungumza kwenye Tafrija ya Walimu Manispaa ya Shinyanga.

Na Josephine Charles, SHINYANGA.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Bw. Jomaary  Satura, ameahidi kujenga mabweni sita kwa shule za sekondari za Mwamalili,Mwawaza na Kizumbi, ambapo kila shule itakuwa na mabweni mawili, lengo likiwa ni kupunguza changamoto za wanafunzi kutembea umbali mrefu kwenda kusoma, pamoja na kuchochea ufaulu kwa wanafunzi wa shule hizo.

Hayo ameyabainisha katika tafrija ya usiku wa waalimu ambayo yamefanyika katika ukumbi wa Lyakale hotel mjini Shinyanga, ambapo pamoja na mambo mengine waalimu  na watumishi mbalimbali wa manispaa ya shinyanga, walipata wasaa wa kujitathmini,kupima mafanikio,kupongezana pamoja na kupanga mikakati ya kazi zao.

Amesema kwa mwaka huu wa fedha 2021/2022 kwa kuanza watajenga mabweni sita ambayo yatagharimu kiasi cha zaidi ya shilingi million 800 ambayo kimsingi hayapo kwenye bajeti waliyonayo lakini ameahidi kutafuta pesa ili kuweza kuwanusuru wanafunzi pamoja na kurahisisha kazi kwa waalimu.

Mkurugenzi huyo amezungumzia changamoto ya watoto kukaa chini kwa kukosa madawati na wengine kwenda shule na viti vyao,hivyo amesema kabla serikali kuu haijaeleza kusapoti katika eneo hilo,halmashauri ya manispaa ya shinyanga walishatenga shilingi million 300 na kuingia mkataba na VETA kutengeneza viti na meza 2500 kwa ajili ya wanafunzi wa sekondari pamoja na kutengeneza madawati 2500 kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya msingi.

Amezungumzia pia uchakavu wa miundominu ya madarasa katika baadhi ya shule za msingi na amesema kuwa kutajengwa madarasa matano mapya katika shule ya msingi Ugweto iliyopo kata ya Ibadakuli kwa kuwa zina nyufa nyingi pamoja na shule ya msingi Kolandoto,Iwelyangula,Bugimbagu na Seseko.

Amesema zoezi la kujengwa majengo mapya ya madarasa katika shule hizo litaenda sambamba na ukamilishaji wa miundombinu ya sekta ya afya kwa maana ya Zahanati kwa kuwa huduma hizo hazipo moja kwa moja na ameeleza zaidi kwamba ikiwa yeye ni mwajiri anatamani kuona mazingira ya watumishi wenzake wanayofanyia kazi yanakuwa bora pamoja na maisha yao yanakuwa bora ingawa kutakuwa na changamoto kubwa katika utekelezaji wake kwa kuwa halmashauri ya manispaa ya shinyanga ina watumishi takriban 1507 ambapo zaidi ya asilimia 50 ni waalimu.

Mkurungenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura, akikata keki kwenye Tafrija wa Walimu Manispaa ya Shinyanga.

Baadhi ya walimu wakitoa Burudani.

Post a Comment

0 Comments