Wananchi wakishirikiana na Jeshi la Polisi kuubeba mwili wa Marehemu
Wananchi wakiangalia mwili wa Kijana Joseph Mushi, akiwa amefariki mara baada ya kuanguka na Pikipiki kwenye Mtaro.
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
Kijana Joseph Mushi mkazi wa Ndembezi Manispaa ya Shinyanga, amefariki dunia mara baada ya kuanguka na pikipiki kwenye Mtaro uliopo eneo la Buluba darajani Kata ya Ngokolo Manispaa ya Shinyanga.
Tukio hilo limetokea leo Jumatatu Oktoba 11,2021 majira ya saa 11 jioni, wakati kijana huyo akitokea maeneo ya Ndembezi kwenda katikati ya Mji wa Shinyanga, alipofika eneo hilo ndipo akapata ajali na kufariki dunia papo hapo.
Mashuhuda wa ajali hiyo ,akiwemo Bugegena Thomas, wamesema walimuona kijana huyo akiwa mwendokasi, lakini ghafla pikipiki yake yenye namba za usajili MC 219 BRP, ilimshinda kukata kona na kisha kuanguka ndani ya mtaro na kufariki dunia.
"Sisi ni mafundi pikipiki ambao tupo hapa kijiweni, tumemuona kijana huyu akipita hapa akiwa Spidi kali ,lakini kona ilimshinda na kwenda kuanguka kwenye mtaro, na kujipiza kwenye nguzo ya taa barabarani, na kuchanika kichwa, sababu hakuwa na kofia ngumu kichwani (HELMET), na kuanza kumwaga damu nyingi," amesema Thomas.
Aidha, Jeshi la Polisi limefika eneo la tukio, na kisha kuuchukua mwili wa marehemu, na kuupeleka kwenye chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Rufa ya mkoa wa Shinyanga.
0 Comments