Header Ads Widget

RAIS MWINYI ATEMBELEA BANDA LA TIC NA ZIPA... AWAPONGEZA KWA USHIRIKIANO NA KUIMARISHA UWEKEZAJI TANZANIA


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ametembelea banda la Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) katika Maonesho ya kwanza ya Utalii ya Kikanda ya Jumuia ya Afrika Mashariki na kuwapongeza kwa ushirikiano walionao katika kuimarisha Uwekezaji Tanzania.

Rais Mwinyi ameyasema hayo alipofika kufunga maonesho hayo.

Rais Mwinyi amewaalika wawekezaji kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na nyingine duniani kuja kuwekeza Zanzibar na Tanzania Bara.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa ZIPA Bw. Shariff A. Shariff amemshukuru Rais Mwinyi kwa kupita kwenye banda la taasisi za uwekezaji hizo mbili na kumhakikishia kuendelea kushirikiana vizuri ili kuendelea kukuza na kurahisisha uwekezaji Tanzania.
Meneja wa Kanda ya Kaskazini (TIC) Bw. Daudi Riganda akiwa pamoja na wawekezaji wa kampuni ya Range Safari waliofika kwenye banda la maonesho kuishukuru TIC kwa kurahisisha shughuli zao za Uwekezaji nchini kwenye maonesho ya kwanza ya Utalii ya kikanda ya Jumuiya ya Africa mashariki yanayofanyika mkoni Arusha leo tarehe 11 Oktoba, 2021.

Kaimu Meneja wa Idara ya Huduma kwa Wawekezaji Bw. George Mukono akiwahudumia wateja waliofika kwenye banda la TIC na ZIPA kujua namna ya kuwekeza kwenye sekta ya elimu katika maonesho ya kwanza ya Utalii ya kikanda ya Jumuiya ya Africa mashariki yanayofanyika mkoni Arusha leo tarehe 11 Oktoba, 2021.

Post a Comment

0 Comments