Header Ads Widget

KAHAMA JOGGING WAJIANDAA KUWAKABILI SHINYANGA JOGGING.


Kuelekea Mashindano ya Michezo mbalimbali itakayofanyika uwanja wa Manispaa Kahama Jumapili ya October 17 club ya ya mazoezi ya Kahama Jogging, imeanza maandalizi ya kuwakabili Club ya Michezo kutoka Shinyanga itwayo Shinyanga Jogging.

Akioongea na Kahama Fm mara baada ya mazoezi ya asubuhi ya leo Mwenyekiti wa Kahama Jogging Hussen Salumu amesema kuwa Kahama Jogging imejipanga kushinda michezo yote kwani washiriki wamejitoa kwa moyo wote kuhakikisha wanashinda katika michuano hiyo.

Salumu amesema kuwa wanawatambua Shinyanga Jogging kwa muda mrefu na kwamba mashindano ya Jumapili wasitegee ushindi wowote kwani mazoezi wanayoendelea nayo ni makali yakuhakikisha ushindi unabaki Kahama.

Akielezea mazoezi yaliyofanyika leo Katibu wa Kahama Jogging Yusuph Makombe amesema kuwa leo wamekimbia umbali wa km 10 kukimbia kwenye magunia na kuvuta kamba sanjali na kufanya mazoezi ya viungo.

Nao baadhi ya wanachama wa Kahama Jogging Steve Cleophace na Lubango Yusuph wamesema kuwa wamejipanga vizuri kushindana na Shinyanga Jogging na kwamba mazoezi yote wanayotolewa na walimu wanayazingatia huku wakitoa salamu kwa wapinzani wao kujiandaa kikamilifu.

Kahama Jogging inatarajia kuwakaribisha Shinyanga Jogging siku ya jumapili October 17 katika uwanja wa Manispaa Kahama kushindana michezo mbalimbali ikiwemo Mbio za kawaida na mbio za magunia,Kuvuta kamba,Mpira wa miguu,Mpira wa pete pamoja na michezo mingine.


Mazoezi yakiendelea.


Post a Comment

0 Comments