Header Ads Widget

MANARA, CEO WAUZUNGUMZIA MCHEZO WA AS VITA, WAUPA JINA LA 'DO OR DIE: SEASON TWO'

Mtendaji Mkuu wa Simba SC, Barbara Gonzalez

"Leo tumepata habari njema kutoka CAF kuwa tumeruhusiwa mashabiki 10,000 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita Club."- CEO Barbara.

"Hii ni fursa ya kipekee ambayo tumeipata. Hakuna timu imeruhusiwa kwa idadi hii. Masharti ni mengi na lazima tuzingatie taratibu walizoweka."- CEO Barbara.
Afisa Habari wa Simba SC, Hajji Manara

"Kwa mashabiki wetu watu 10,000 ni watu wachache sana. Hatutarajii siku ya mchezo watu wawe bado hawajanunua tiketi sababu siku ya mchezo CAF hawaruhusu tiketi kuuzwa uwanjani."- Manara.

"Hakuna namna lazima tupate ushindi kwenye mchezo huu. Hii itakuwa ni DO OR DIE; SEASON TWO na hiyo ndio itakuwa kauli mbiu yetu."- Manara.

"Kikosi chetu kipo vizuri wachezaji wengine wameshawasili na wengine wanaendelea kuwasili. Afya za wachezaji zipo vizuri tofauti na zinavyoandikwa baadhi ya sehemu na tutaendelea kuchukua hatua."- Manara

Credit: Simba SC TanzaniaPost a Comment

0 Comments