Header Ads Widget

WAZIRI AWESO AONYA MRADI WA MAJI TINDE NA SHELUI WA SH. BILIONI 24 KUHUJUMIWA


Waziri wa maji Jumaa Aweso, akizungumza kwenye zoezi la utiaji saini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji ziwa victoria, ambao utatekelezwa katika mji wa Tinde wilayani Shinyanga na Shelui wilayani Ilamba, kwa gharama ya Sh. Bilioni 24.4

Na Marco Maduhu - SHINYANGA 
WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amewaonya wananchi wa Mji wa Tinde wilayani Shinyanga pamoja na Mji wa Shelui wilayani Ilamba mkoani Singida, wasihujumu ujenzi wa mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria ambao utatekelezwa kwenye miji hiyo kwa gharama ya Sh. Bilioni 24.4. 

Waziri Aweso ametoa onyo hilo leo katika mji mdogo wa Tinde wilayani Shinyanga wakati wa utiaji saini wa mkataba wa ujenzi  wa mradi huo wa maji kutoka Ziwa Victoria utakaopelekwa kwenye miji ya Tinde na Shelui, ambao ulisainiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Athony Sanga na Mkandarasi ambaye ataujenga mradi huo Morali Mohani, kutoka kampuni ya Megha Engeneering Construction ya nchini India. 

Amesema fedha ambazo zinatekeleza mradi huo ni nyingi, na kuwaomba ushirikiano wananchi wa maeneo ambao unatekelezwa mradi huo, wasihujumu mradi wala kuiba vifaa vya ujenzi, bali wautunze vizuri ili upate kuwatatulia kero ya ukosefu wa maji safi na salama. 

“Mradi huu wa maji safi na salama utawasaidia kuondokana na adha ya kutafuta maji salama umbari mrefu, pamoja na kupoteza muda wa kufanya shughuli za kiuchumi hivyo naomba muutunze,” amesema Aweso na kuongeza. 

“Huu ni mradi wangu wa kwanza kusainiwa nikiwa Waziri wa Maji, nawaomba Wakandarasi vipo vya kuchezea lakini siyo mradi huu, umalizeni kwa wakati na hakutakuwa na muda wa nyongeza,”

Pia amewaagiza wakandarasi wakati wa kuutekeleza mradi huo, vijana ambao ni wakazi wa Tinde na Shelui ndio watakao pewa kazi na siyo kutoka maeneo mengine, ili wapate vipato na kuinuka kiuchumi. 

Aidha amezitaka mamlaka za maji ambazo zitakabidhiwa kuendesha mradi huo pale utakapo kamilika na kusambaza huduma ya maji kwa wananchi, wasitoze bili kubwa za maji, bali wafuate viwango vya bili ambazo zinasimamiwa na mamlaka ya udhibiti ubora wa nishati na maji Ewura. 

Katika hatua nyingine, Waziri Aweso aliwaonya wahandisi wa maji hapa nchini, kuacha kufanya kazi kizembe, bali wajitume na kufanya kazi kwa weledi, ambapo watendaji wa namna hiyo hatowavumilia, na kubainisha mpaka sasa wamesha fukuzwa Wahandisi 100. 

Naye Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga, amesema fedha za utekelezaji wa mradi huo wa Sh. Bilioni 24.4 ni fedha za mkopo wa mashariti nafuu kutoka nchini India kupitia benk ya Exim, na kuonya kwenye mradi huo hakutakuwa na gharama za nyongeza bali fedha zilizotolewa ndio zitatumika kuukamilisha. 

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack, ameshukuru Rais Dk. John Magufuli kwa kutekeleza ahadi yake ya kupeleka huduma ya maji safi na salama kwa wananchi wa Tinde, na kuahidi Serikali kutoa ushirikiano kwa Mkandarasi huyo ili asipate vikwazo vyovyote wakati wa utekelezaji. 

Aidha Mbunge wa Jimbo la Solwa Ahmed Salum, amesema kwenye utekelezaji wa mradi huo wa maji vitanufaika vijiji 33, na hivyo kufanya Jimbo hilo hadi kufikia mwaka 2025, asilimia 95 ya wananchi watakuwa wakitumia maji safi na salama jimboni humo. 

Nao baadhi ya wananchi ambao walihudhulia kwenye utiaji saini wa mradi huo mkubwa wa maji, akiwamo Happnes Makoye mkazi wa Tinde, amesema mradi huo utawasaidia kuondokana na shida ya kuamka mida ya usiku kufuata maji umbari mrefu, pamoja na kupoteza muda wa kufanyashughuli za kiuchumi. 

TAZAMA PICHA ZA TUKIO HILO HAPA CHINI
Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Athony Sanga (kushoto) na Mkandarasi Morali Mohani kutoka kampuni ya Megha Engeneering Constraction ya nchini India, wakitia saini za mkataba wa ujenzi wa mradi huo wa maji ambao utatekelezwa katika mji wa Tinde na Shelui.


Waziri wa maji Jumaa Aweso, akizungumza kwenye utiaji wa siani ujenzi mradiwa maji ziwa victoria ambao utakelezwa katika mji wa Tinde wilayani Shinyanga na Shelui wilayani Ilamba.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Athony Sanga, akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo wa maji kutoka ziwa victoria katika mji wa Tinde na Shelui.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, akizungumza kwenye utiaji saini mkataba wa utekelezaji wa mradi huo wa maji.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza kwenye zoezi hilo la utiaji saini mkataba wa mradi wa maji ziwa victoria ambao utatekelezwa katika mji wa Tinde na Shelui.
Mkuu wa wilaya ya Ilamba Emmanuel Ruhahula, akizungumza kwenye utiaji saini mkataba wa mradi wa maji ya ziwa victoria, ambao utakelezwa katika mji wa Tinde na Shelui.
Mbunge wa Jimbo la Solwa Ahmed Salum akizungumza kwenye utiaji saini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji ziwa victoria ambao utatekelezwa katika mji wa Tinde na Shelui.
Mbunge wa vitimaalu mkpani Shinyanga Christina Mzava, akizungumza kwenye zoezi la utiaji saini wa mradi wa maji ziwa victoria ambao utatekelezwa katika mji wa Tinde na Shelui.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Athony Sanga kushoto, akiwa na Mkandarasi ambaye ataujenga mradi maji Morali Mohani, kutoka kampuni ya Megha Engeneering Constraction ya nchini India, wakitia saini za mkataba wa ujenzi wa mradi huo wa maji ambao utatekelezwa katika mji wa Tinde na Shelui.
Viongozi wakishuhudia zoezi hilo la utiaji saini mkataba wa ujenzi mradi wa maji.
Wananchi wakishuhudia zoezi hilo la utiaji saini mkataba wa utekelezaji wa mradi wa maji katika mji wa Tinde na Shelui.
Wananchi wakishuhudia zoezi hilo la utiaji saini mkataba wa utekelezaji wa mradi wa maji katika mji wa Tinde na Shelui.
Wananchi wakishuhudia zoezi hilo la utiaji saini mkataba wa utekelezaji wa mradi wa maji katika mji wa Tinde na Shelui.
Wananchi wakishuhudia zoezi hilo la utiaji saini mkataba wa utekelezaji wa mradi wa maji katika mji wa Tinde na Shelui.
Wananchi wakishuhudia zoezi hilo la utiaji saini mkataba wa utekelezaji wa mradi wa maji katika mji wa Tinde na Shelui.
Zoezi la utiaji saini mktaba wa ujenzi wa mradi wa maji ukiendelea kushuhudiwa.
Zoezi la utiaji saini mktaba wa ujenzi wa mradi wa maji ukiendelea kushuhudiwa.
Zoezi la utiaji saini mktaba wa ujenzi wa mradi wa maji ukiendelea kushuhudiwa.
Zoezi la utiaji saini mktaba wa ujenzi wa mradi wa maji ukiendelea kushuhudiwa.
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso (watatu kutoka kulia), akipiga picha ya pamoja na viongozi mara baada ya zoezi la utiaji saini mkataba wa ujenzi mradi wa maji kukamilika ambao utatekelezwa katika Mji wa Tinde na Shelui, watatu kutoka kushoto ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, na wapili kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Atthony Sanga.akiwa jirani na katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Albert Msovela.
Waziri wa Maji Jumaa Aweso, watatu kutoka kulia, akipiga picha ya pamoja na viongozi mara baada ya zoezi la utiaji saini mkataba wa ujenzi mradi wa maji kukamilika ambao utatekelezwa katika Mji wa Tinde wilayani Shinyanga na Shelui wilayani Ilamba.

Picha zote na Marco Maduhu


Post a Comment

0 Comments