Header Ads Widget

MAFURIKO MTWARA, DC NA MKURUGENZI WAWATAKA WANANCHI KUJIHIFADHI SHULENI

Hali ilivyo katika Manispaa ya Mtwara kutokana na mvua kubwa inayonyesha tangu asubuhi leo (Picha zote: Millardayo)

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Dunstan Kyobya amewaomba Wananchi wote wanaoishi bondeni na maeneo yote yaliyoathiriwa na mvua zinazoendelea kunyesha Mtwara Mjini wasogee maeneo ya karibu na Shule za Sekondari na Msingi zilizopo maeneo ya juu kwa msaada zaidi.

Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Mtwara zimesababisha athari katika maeneo mbalimbali ikiwemo Barabara, Stendi kuu ya Mabasi na Soko Kuu ambako kote kumejaa maji na baadhi ya nyumba za watu pia zimeathiriwa.

Kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha ndani ya Mji wa Mtwara, Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani, Kanali Emmanuel Mwaigobeko amewataka Wananchi wote wanaoishi bondeni na sehemu zenye mafuriko kuondoka mara moja na kuelekea kwenye maeneo ya shule zilizopo jirani na maeneo wanayoishi.Shule zilizoandaliwa ni Shule za Sekondari za Mikindani, Mitengo, Mangamba, Sino, Chuno, Shangani, Rahaleo, Bandari, Umoja na Naliendele huku Shule za Msingi zilizondaliwa zikiwa ni Majengo, Tandika, Rahaleo, Kambarage na Lilungu.

“Taarifa hii ni ya muhimu sana hivyo Wananchi wote wanatakiwa kuchukulia kwa uzito wa kipekee”
Picha mbalimbali zikionyesha hali ilivyo katika Manispaa ya Mtwara-Mikindani kutoka na Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha leo

Post a Comment

0 Comments