Header Ads Widget

MAWAZIRI WAWILI MALAWI WAFARIKI KWA CORONA

Lingson Belekanyama alipatikana na Covid-19 wiki iliyopita.

MALAWI leo Januari 12, 2021 imepata pigo baada ya mawaziri wawe wawili kufariki dunia kutokana na Covid-19.

Waziri wa Habari wa Malawi, Gospel Kazako, amethibitisha kuwa mawaziri hao ambao ni Waziri wa Serikali za Mitaa, Lingson Belekanyama na Waziri wa Uchukuzi, Sidik Mia, wamefariki ndani ya saa mbili.


Mwishoni mwa juma, Rais wa nchi hiyo, Lazarus Chakwera, alitoa hotuba maalumu kwa njia ya radio kwa taifa akitoa wito wa kuheshimiwa kwa hatua zilizowekwa za kupambana na maambukizi ya Covid-19 kufuatia ongezeko kubwa katika vifo na maambukizi ya virusi hivyo. Chakwera anatarajiwa kutoa hotuba nyingine kwa taifa baadaye leo, kwa mujibu wa Kazako.




Post a Comment

0 Comments