Header Ads Widget

WALIMU WAWILI HATIANI KWA MAUAJI SHULENI

Watuhumiwa Leah Agunda na Martha Laizer wakiongozana na askari kurudi rumande

Walimu wawili waliofahamika kwa majina ya Leah Agunda na Martha Laizer, leo Novemba 6, 2020 wamefikishwa mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam wakikabiliwa na kosa la mauaji.

Washtakiwa wote kwa pamoja wanadaiwa kutenda kosa hilo mnamo Septemba 14,2020 katika shule ya awali na msingi Holy Cross iliyopo Kijichi Jijini Dar es salaam kwa kumuuwa Cathbert Felix Chawe.

Aidha Hakimu Luborogwa amesema kutokana na makosa yanayowakabili washtakiwa hao, hawakutakiwa kujibu chochote hivyo wamerudishwa rumande na kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 19, mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments