Header Ads Widget

MBUNGE WA ZAMANI MOSHI VIJIJINI, DK. CYRILI CHAMI AFARIKI DUNIA


Marehemu, Dk. Cyril Chami

Aliyewahi kuwa Mbunge wa Moshi Vijijini, Dr. Cyrili Chami, amefariki dunia usiku wakuamkia leo Novemba 5, 2020, katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, jijini Dodoma, alipokuwa amelazwa kwa matibabu.

Dk. Chami alihudumu kama mbunge wa Moshi Vijijini kuanzia mwaka 2005, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akiwa Mbunge, Rais wa Awamu ya nne, Jakaya Kikwete, alimeteua Januari 4, 2006, kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje.

Alihuduma katika Wizara hiyo ya Mambo ya Nje kabla ya Februari 12, 2008, kuhamishwa na kuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara kabla ya kuwa Waziri kamili wa Wizara hiyo kuanzia mwaka 2010 hadi 2012.

Post a Comment

0 Comments