Header Ads Widget

AMUUA MKEWE, NAE AJIKATA UUME BAADA YA NYUMBA KUUZWA, MWINGINE AMUUA ALIYEMFUKUZA HARUSINI


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara ACP Daniel Shillah amethibitisha kushikiliwa kwa mwanaume mmoja anayetambulika kwa jina la Masunga Ngilama (25) Mkazi wa Mpanda mkoani Katavi kwa kuumuua mke wake Shida Maduhu (25) Mkazi wa Bunda kwa kumchinja kwa kisu kisha naye kujikata sehemu zake za siri.

Kamanda amesema Mwanaume huyo alienda kutafuta maisha Zanzibar na aliporudi alikuta Mkewe amehama na kuuza kila kitu ikiwemo nyumba waliyokuwa wanaishi “alifuatilia huko Bunda ili wapate suluhu lakini Mwanamke alikataa”

“Wakiwa Bunda wawili hao walienda kutembea nje ya Kijiji chao, ndipo Mwanaume alipomshambulia kwa kumchinja Mkewe na kusababisha kifo, nae alijikata sehemu za sehemu akitaka kujiua” RPC Mara

Jamaa amuua aliemfukuza harusini
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara linamshikilia kijana mmoja anayetambulika kwa jina la Nchagwa Sasi (18) Mkazi wa Kijiji cha Malenga katika Wilaya ya Serengeti kwa kosa la kumuua Kegoka Mwikabe (20) baada ya marehemu kumfukuza kwenye harusi ya rafiki yao kutokana na kutokuwa na zawadi.

“Tumemkamata Mchagwa ambaye ni mkulima kwa kosa la mauaji, awali wawili waliudhuria sherehe, huyu marehemu alikuwa anasimamia kamati ya Vijana wenzake iliyokuwa inahusika na suala la kutoa zawadi, ndipo walibaini mshatakiwa hakuwa na zawadi, ndipo Marehemu alipoamua kumtoa nje” RC Mara.

Post a Comment

0 Comments