Header Ads Widget

PICHA: JPM, MAMA JANETH, DK. SHEIN, MAMA SAMIA, MAJALIWA, MWINYI NA MAALIM SEIF WALIVYOPIGA KURA

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli akipiga kura

Akizungumza baada ya kupiga kura, Magufuli amesema; “Napenda niwapongeze wasimamizi wa uchaguzi hapa Chamwino; maandalizi yalikuwa mazuri na watu wamejitokeza kwa wingi, wito wangu kwa Watanzania tujitokeze kwa wingi kupiga kura pia nipende kusisitiza amani.”
Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Magufuli amefika katika kituo chake cha kupigia kura Chamwino Ikulu na kupiga kura yake mapema asubuhi hii.
Dk. John Magufuli akipiga kura
Mama Janeth akipiga kura
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika foleni ya kupiga kura kwa ajili ya kuchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Zanzibar, Wabunge, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani katika kituo cha SOS Mombasa Zanzibar kwenye Uchaguzi Mkuu unaofanyika leo Octoba 28,2020.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea karatasi za kupiga kura kutoka kwa Muwandishi Yussuf Haji katika kituo cha SOS Mombasa Zanzibar kwa ajili ya kupiga kura kuchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Zanzibar, Wabunge, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani kwenye Uchaguzi Mkuu unaofanyika leo Octoba 28,2020.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipiga kura katika kituo cha SOS Mombasa Zanzibar (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika foleni akisubiri zamu yake kwa ajili ya kupiga kura yake kuwachagua Rais wa Zanzibar,Rais wa Tanzania Mbunge.Mwakilishi na Diwani , akiwa katika Kituo cha Kupigia Kura Skuli ya Bungi Wilaya ya Kati Unguja.leo 28/10/2020.
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein wa tatu akiwa katika foleni akisubiri zamu yake kwa ajili ya upigaji wa kura katika Kituo cha kupigia Kura Skuli ya Bungi Wilaya ya Kati Unguja
Dk akipiga kura

Waziri Mkuu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa amepiga kura kijijini kwake Nandagala, wilayani Ruangwa, mkoani Lindi.

Akizungumza mara baada ya kupiga kura, Waziri Mkuu amesema zoezi la kupiga kura ni haki ya msingi na anamshukuru Mungu kwamba limeenda salama. “Ninamshukru Mungu nimeweza kushiriki haki yangu ya msingi ya kumchagua kiongozi ninayempenda ili aweze kuliongoza Taifa hili,” amesema.
Mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad, akipiga kura hii leo visiwani Zanzibar.
Mgombea Urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi akipiga kura leo visiwani humo

Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, akipiga kura katika eneo la Kilimani, jijini Dodoma.

Post a Comment

0 Comments