Header Ads Widget

MAMA WA BEN POL APATA MSHTUKO, ADAI MWANAE HAKUMPA TAARIFA YA KUBADILI DINISIKU chache baada ya msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Bernard Paul ‘Ben Pol’ kuposti picha kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa kwenye mavazi rasmi ya Kiislam, hatimaye mama yake mzazi, Cecilia Buhondo amepatwa na mshtuko.

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA WIKIENDA, mama huyo kwa njia ya simu alisema kwamba, hata yeye mwenyewe alipooneshwa picha hizo alishtuka kwa sababu hakupewa taarifa na kijana wake huyo.

IJUMAA WIKIENDA: Heshima yako mama…

MAMA BEN: Marahaba…

IJUMAA WIKIENDA: Tumeona picha za mwanao Ben zikisambaa kama moto wa kifuu mtandaoni kuwa amebadili dini, hii inakuwaje ilihali ni miezi michache tu iliyopita alitoka kufunga ndoa ya Kikristo?

MAMA BEN: Mimi mwenyewe hapa nimechanganyikiwa kwa sababu nimeona jana tu, hajaniambia kitu chochote, nimeshtuka sana na bado sijaongea naye kitu chochote, lakini nitamtafuta ili aniambie ni kitu gani alichokiamua.

IJUMAA WIKIENDA: Ina maana hata simu hujampigia kumuuliza kulikoni? MAMA BEN: Nilimpigia sana simu yake, lakini iliita tu bila kupokelewa, nadhani labda anahitaji muda wa kupumzika mwenyewe, hivyo hataki kusumbuliwa.

IJUMAA WIKIENDA: Vipi kwani bado yupo na mke wake, Anerlisa?

MAMA BEN: Ndiyo bado wapo pamoja, ila mwanamke amesafi ri, ana kama wiki moja yupo safarini.

IJUMAA WIKIENDA: Na yeye mkwe wako hujamtafuta ili kujua lolote?

MAMA BEN: Bado sijamtafuta, nataka niongee kwanza na Ben mwenyewe. Ishu ya msanii huyo kuonekana amebadili dini iliwafanya baadhi ya mashabiki, kila mmoja kuanza kuongea lake huku baadhi yao wakisema kuwa, kwa sasa itakuwaje kuhusu ndoa aliyofunga na Anerlisa?

“Jamani kama kweli Ben amebadili dini, ina maana ile ndoa yao ya kwanza ni batili? Au ameachana na mke wake ndiyo maana ameamua kubadili dini?” Hayo ni baadhi ya maswali aliyouliza shabiki mmoja kwenye Instagram bila kupata majibu.

“Mmmh! Huyu naye anatuchanganya, juzi tu ametoka kufunga ndoa ya Kikristo, hivi si anacheza na dini za watu huyu?”

Alihoji shabiki mwingine. Hata hivyo, kwa madai yaliyopo, inasemekana kwamba, Ben Pol alibadili dini siku ya Ijumaa ya Oktoba 23, mwaka huu katika Msikiti wa Maamur uliopo Upanga jijini Dar na sasa anaitwa Behnam.

Hata hivyo, wananzengo wanasema kuwa, msanii huyo tayari ameshaachana na mke wake, Anerlisa Muigai hivyo kwa sasa amepata mchumba mwingine aitwaye Khairat.

Gazeti la IJUMAA pia halikuishia hapo, lilifanya jitihada za kumtafuta Ben Pol mwenyewe ili azungumzie ishu hiyo ambapo simu yake iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa.

Post a Comment

0 Comments