Header Ads Widget

BREAKING NEWS: MGOMBEA UBUNGE SHINYANGA MJINI AKAMATWA NA POLISI USIKU

Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Salome Makamba akizungumza na wananchi katika moja ya mikutano yake ya kampeni jimboni humo

Na Marco Maduhu, Shinyanga
JESHI la Polisi mkoani Shinyanga linamshikilia Mgombea Ubunge wa Jimbo la Shi nyanga Mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Salome Makamba kwa tuhuma za kumshambulia msimamizi wa uchaguzi kituo cha kupigia kura cha Bugweto B, Farida John na kumuumiza vibaya.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Debora Magiligimba imesema kuwa tukio hilo limetokea Oktoba 28, mwaka huu saa 2 usiku , ambapo Makamba aliomba aone matokeo na baada ya kutoridhika nayo aliyachana na kuanza kumshambulia msimamizi huyo wa uchaguzi akiwa na wafuasi wake.

ACP Magiligimba amesema baada ya kupata taarifa za tukio hilo, jeshi la polisi lilimsaka mtuhumiwa na kumkamata, ambapo kwa sasa yupo mahabusu (sero) na upelelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.

Post a Comment

0 Comments