Header Ads Widget

MGOMBEA AELEZA SABABU YA KUMNUNULIA JPM KEKI

Kushoto ni mgombea ubunge wa jimbo la Ubungo, Profesa Kitila Mkumbo, na kulia ni mgombea Urais Dkt John Pombe Magufuli.

Mgombea ubunge wa jimbo la Ubungo kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Profesa Kitila Mkumbo, amesema kuwa mara baada ya kupiga kura, ataenda Mlimani City kumnunulia mgombea Urais wa chama hicho Dkt. John Magufuli, keki ya 'birthday', kwa lengo la kumtakia heri na mafanikio.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Oktoba 28, 2020, mara baada ya kukamilisha zoezi lake la upigaji wa kura, na kuahidi jambo hilo.

"Katika kutimiza miaka yake 61 nimnunulie keki, nimtakie afya njema na nimtakie mafanikio makubwa katika kuongoza Tanzania kwa awamu yake ya pili", amesema Profesa Kitila.

Zoezi la upigaji wa kura nchini Tanzania limeanza leo Oktoba 28, 2020, saa 1:00 asubuhi na kuhitimishwa saa 10:00 jioni na kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi jumla ya Watanzania Milioni 29 walikuwa wamejiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura.

Post a Comment

0 Comments