Header Ads Widget

SHY SUPER QUEENS YAIKUNG'UTA VIVA QUEENS 16-0, MESSI AFUNGA 10

Timu ya Shinyanga Super Queens

Na Shinyanga Press Club Blog
TIMU ya Shinyanga Super Queens imeendelea kuonyesha makali kwenye michuano ya Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara kwa Soka la Wanawake, baada ya kucheza michezo mitatu mfululizo bila kufungwa.

Katika michuano hiyo inayofanyika jijini Dodoma kwenye viwanja vya Puma na Fountain Gate, Shinyanga Super Queens ambayo inasaka nafasi ya kucheza Ligi Kuu msimu ujao ilianza kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mkwawa Queens.

Katika mchezo wa Pili kwenye kundi lao la C uliochezwa jana dhidi ya Mt. Hanang ya Manyara, Vijana wa Shinyanga walilazimishwa sare ya mabao 3-3.

Leo mapema asubuhi ya Septemba 2, 2020, Shinyanga Super Queens imetoa kipigo cha mbwa mwizi kwa wapinzani wao wa Viva Queens baada ya kuishushia mvua ya mabao kwa kuikung'uta magoli 16-0 na kuzidi kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo.

Mabao ya Shinyanga Super Queens yalifungwa na Mshambuliaji wao hatari, Irine Chitanda aliyepachikwa nyavuni magoli 10 peke yake, mabao mengine yalifungwa na wachezaji Patricia Salum(2), Nyanyama George (1), Tatu Abbas (2) na Neema George (1)