Header Ads Widget

WASICHANA WENYE UJAUZITO KUPEWA ELIMU YA LISHE MANISPAA YA SHINYANGA
Wasichana wenye ujauzito na wale wenye watoto walio na umri wa miaka sita manispaa ya Shinyanga, wanatarajiwa kupewa elimu ya lishe bora kwa watoto, ili kupunguza tatizo la udumavu na utapiamlo.
Afisa mradi kutoka Shirika la WEADO linalotetea haki za watoto, wanawake, na wazee mkoani Shinyanga Immaculate Komba, alibainisha hayo jana wakati akitambulisha mradi wa wajibu wa wazazi kutekeleza majukumu yao kwa watoto likiwamo suala la lishe, utakaotekelezwa kwenye Kata ya Chibe manispaa ya Shinyanga kwa ufadhili wa Firelight Foundation.

Alisema wasichana wenye ujauzito na walio na watoto wenye umri wa miaka sita, wengi hawana elimu ya malezi na makuzi ya watoto, likiwamo na suala lishe bora, hali ambayo inasababisha watoto wao kukumbwa na tatizo la udumavu na utapiamlo.

Shirika letu la WEADO tutatekeleza mradi wa wajibu wa wazazi kutekeleza majukumu yao kwa watoto, likiwamo suala la Lishe bora, ambao utakoma june 2021 kwa gharama ya Shilingi 18,468,000, walengwa wetu wakuu ni wasichana wenye ujauzito, na wenye watoto wa umri wa miaka sita ,” alisema Komba.

Pia mabinti hawa tutawapatia elimu ya ujasiriamali pamoja na kuwaunga kwenye vikundi, ili wapate fedha za mitaji kupitia asilimia 10 ya halmashauri, na kuanzisha biashara mbalimbali ambazo zitawakwamua kiuchumi, na hatimaye kukidhi mahitaji ya familia zao na kuwahudumia watoto,: aliongeza.

Naye mkurugenzi wa Shirika hilo la (WEADO) Eliasenya Nnko, alisema madhumuni ya kuanzisha mradi huo ni kuwakumbusha wazazi juu ya majukumu yao ya malezi bora kwa watoto likiwamo suala la lishe, ili kuwa na jamii salama kiakili na kiuchumi.
Afisa lishe manispaa ya Shinyanga Joanita Jovini, alisema tatizo la udumavu kwa watoto lipo asilimia 32, na kubainisha Serikali bado inaendelea kutoa elimu kwa wazazi kuzingatia suala la lishe bora kwa watoto.

Kwa upande wake mgeni rasmi mratibu wa mfuko wa maendeleo ya jamii wa kunusuru Kaya maskini (TASAF) manispaa ya Shinyanga Octavina Kiwone, akimwakilisha afisa maendeleo ya jamii manispaa hiyo, alisema mradi huo umekuja muda muafaka, ambapo wasichana wengi hawajui namna ya malezi bora ya watoto.

Aidha alisema Serikali itashirikiana kikamilifu na Shirika hilo kutoa elimu ya makuzi, matunzo, lishe bora kwa watoto, pamoja na kutokomeza tatizo la mimba za utotoni ambalo limekuwa changamoto kubwa mkoani Shinyanga, na kusababisha ukosefu wa malezi bora kwa watoto.

TAZAMA PICHA HAPA CHINIMkurugenzi wa Shirika la WEADO Eliasenya Nnko, akitambulisha mradi.

Afisa Mradi kutoka Shirika la WEADO Immaculate Komba akielezea namna mradi utakavyofanya kazi kwenye Kata ya Chibe.

Mgeni Rasmi akifungua kikao.

Mkurugenzi wa Shirika la Agape John Myola akichangia mada kwenye kikao hicho.

Washiriki wakiwa kwenye kikao.

Washiriki wakiwa kwenye kikao.

Washiriki wakiwa kwenye kikao.

Washiriki wakiwa kwenye kikao.

Washiriki wakiwa kwenye kikao.

Washiriki wakiwa kwenye kikao.

Washiriki wakipiga picha ya pamoja.


Na Marco Maduhu- Shinyanga.