Header Ads Widget

WAFANYABIASHARA SOKO KUU MANISPAA YA SHINYANGA WAIANGUKIA SERIKALI


Mmoja wa wafanyabiashara wa soko kuu mjini Shinyanga bi Regina Peter  akiendelea kufanya shughuli za kuuza bidhaa mbalimbali 

Wafanyabiashara wa soko kuu  manispaa ya Shinyanga wameiomba serikali kukarabati  soko hilo kwa kuweka vifusi vya molamu na mitaro kwa ajili ya kutolea maji pindi inaponyesha mvua ili kuondokana na magonjwa ya milipuko  inayosababishwa na maji machafu yanayotuama ndani ya soko hilo.
 Wakizungumza kwa nyakati  tofauti  wafanyabiashara hao Faustine Magesa na Mariam Samson wamesema wamekuwa wakipatwa hofu kubwa ya kupatwa na magonjwa ya milipuko kama vile kipindupindu na magonjwa mengine pindi inaponyesha mvua kwani maji yamekuwa yakituama hayana sehemu ya kutokea.
Wamesema soko hilo   tangu lianzishwe mwaka 1979 halijawahi kukarabatiwa hivyo wanaiomba serikali iwaonee huruma na kukarabati   soko hilo ili waendelee kufanya biashara kwa amani kwani wamekuwa wakihofia kupatwa na magonjwa ya milipuko.
Tunaiomba  sana serikali yetu ituangalie nasisi hapa tulipo na tunapoona wingu kama hili tunapatwa na hofu kubwa, kwani inaponyesha mvua hali ya humu inatisha, maji yanaelea hayana sehemu ya kwenda, wengi tunaugua fangasi miguuni kwa sababu ya kukanyaga maji machafu na tunakuwa na hofu ya kupatwa na magonjwa ya milipuko”amesema Samson
Tunamuomba tu hata mkurugenzi wetu Geofrey Mwangulumbi aje ajionee mwenyewe hali ilivyo, kwani tumekuwa tukilalamika mara kwa mara lakini hatuoni utekelezaji wake, tunamuomba kipindi hiki atukumbuke na sisi ili tuweze kufanya biashara zetu kwa amani tusihofie magonjwa kila wakati"amesema Magesa.
Mwenyekiti wa soko hilo Alex Stephen amesema kweli wafanyabiashara wanapata shida sana wakati wa mvua kwani maji yanatuama hayana sehemu ya kwenda kutokana na miundombinu ya soko kuwa mibovu.
Manispaa inatakiwa kuja kuangalia miundombinu ya soko hili kwani hairidhishi hata kidogo, tuliwaambia waje watengeneze mitaro ya kupitishia maji na kuweka vifusi ndani ya soko ili maji yasiendelee kutuama, lakini hatujawaona mpaka sasa na soko hili ni la kwanza kujengwa mjini hapa na ni soko kuu”amesema Stephen.
Kwaupande wake mkurugenzi wa manispaa Geofrey Mwangulumbi amesema kweli Kuna shida Katika soko hilo lakini tayari tumeliweka kwenye mpango wa kulikalabati katika bajeti ya mwaka huu.
"Tumeshaliweka kwenye bajeti ya mwaka huu mpya wa fedha kwani tunaijua changamoto iliyopo katika soko hilo"amesema mkurugenzi waanispaa ya Shinyanga Mwangulumbi.
 Mwisho.
 Sanchu Rwekaza aakisubiri wanunuzi wa bidhaa za ndizi