Header Ads Widget

MGOMBEA UDIWANI CCM KATA YA NGOKOLO ACHUKUA FOMU AOMBA USHIRIKIANO KWA WAPIGA KURA

Diwani Mteule wa chama cha mapinduzi Kata ya ngoloko Victor Mkwizu akichukua fomu ya NEC kwa Msimamizi msaidizi wa uchaguzi kata hiyo bi Felister Msemelwa

picha na Suzy Butondo.

Shinyanga. Mgombea udiwani kata ya Ngokolo manispaa ya Shinyanga kupitia chama cha mapinduzi (CCM)Victor Mkwizu baada ya kuteuliwa na halmashauri kuu ya mkoa leo amechukua fomu ya kugombea ili aweze kupeperusha bendera ya chama hicho.

Akipokea fomu za kugombea udiwani kata ya Ngokolo Mkwizu amesema anachukua fomu hizo za kugombea udiwani lakini anahitaji ushirikiano mkubwa kutoka kwa wanachama wote wa chama cha mapinduzi ili waweze kupata ushindi.

"Nashukuru sana viongozi na wanachama wenzangu kwa kunisindikiza kuchukua fomu hii, lakini bado nahitaji msaada wenu ili tuweze kupata ushindi katika chama chetu nawaomba tuungane kwa pamoja ikiwa ni pamoja na wagombea wenzangu wa chama cha mapinduzi ili tuweze kupeperusha bendera ya chama cha mapinduzi ".amesema Mkwizu.

Akikabidhi fomu ya kugombea afisa mtendaji wa kata ya Ngokolo Felister Msemelwa amewataka wagombea wote kufuata maelekezo ya kujaza fomu hiyo wasifanye kinyume wakaharibu utaratibu uliowekwa na serikali.

Msemelwa amesema mpaka soasa wamechukua fomu wagombea wanne ambao ni Victor Mkwizu kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Emmanuel Ntobi kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema), Omari Gindu kupitia Chama Cha (ACT)wazalendo, na Charles Shigino kupitia chama cha (NCCR) Mageuzi.

 Victor Mkwizu mgombea udiwani kupitia chama cha mapinduzi CCM kata ya Ngokolo manispaa ya Shinyanga akikabidhiwa fomu ya kugombea na mtendaji wa kata hiyo Felister Msemelwa katika ofisi  hiyo iliyoko mjini Shinyanga
 Wanachama wa chama cha mapinduzi CCM wakimsindikiza mgombea udiwani kupitia chama hicho kwenda kuchukua fomu ya kugombea udiwani katika ofisi ya mtendaji wa kata hiyo iliyopo manispaa ya Shinyanga.
 Victor Mkwizu mgombea udiwani kupitia chama cha mapinduzi CCM kata ya Ngokolo manispaa ya Shinyanga akikabidhiwa fomu ya kugombea udiwani  na mtendaji wa kata ya Ngokolo Felister Msemelwa ili aweze kupeperusha bendera ya chama cha mapinduzi CCM.
 Victor Mkwizi akisalimiana na wananchi baada ya kumzuia njiani na kumuomba wasalimiane na waweze kumpongeza kwa kupeperusha bendera ya chama cha mapinduzi CCM.
Victor Mkwizi akisalimiana na wananchi baada ya kumzuia njiani na kumuomba wasalimiane na waweze kumpongeza kwa kupeperusha bendera ya chama cha mapinduzi CCM.