Header Ads Widget

RAIA 51 WA ETHIOPIA WAKAMATWA WAKIINGIA NCHINI KINYUE CHA SHERIARaia wa Ethiopia walikamatwa mkoani Pwani 


Jeshi la Polisi mkoani Pwani linawashikilia raia 51 kutoka nchini Ethiopia kwa tuhuma za kuingia nchini kinyume cha sheria.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa amesema, raia hao wamekamatwa Agosti 22 ,2020 majira ya saa 11 alfajiri katika mzani wa magari Msata Halmashauri ya Chalinze Wilaya ya Bagamoyo.

Kamanda Wankyo amesema, raia hao wamekamatwa wakiwa kwenye gari iliyokuwa na namba za usajili T. 246 BBG Scania mali ya Uswege Mwamboma.

Amesema, raia hao walikuwa katika safari kutoka Tanga kuelekea Chalinze wote wakikadiriwa kuwa na miaka kati ya 15- 25.

Hata hivyo watu wawili  wanaodhaniwa kuwa Watanzania ambao walikuwa na raia hao wanadaiwa kukimbia baada ya gari hilo kusimamishwa na Askari katika eneo hilo la Msata.

Kamanda Wankyo amewataka watu hao waliotoroka na kuwatelekeza raia hao wa kigeni kujisalimisha pamoja na mmiliki wa gari hilo ambaye walipata anuani yake iliyoandikwa katika Mlango wa gari hiyo.