Header Ads Widget

SHY SUPER QUEENS YAWACHAPA WANAUME 2-1, DC MBONEKO, WADAU WAKABIDHI MBUZI, FEDHA






Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akiserebuka na wachezaji wa timu ya Shinyanga Super Queens baada ya timu hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya vijana wa kiume wa kituo cha Moroto Academy cha mjini Shinyanga katika mchezo wa kirafiki uliochezwa leo uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

Na Damian Masyenene –Shinyanga

MAANDALIZI ya wawakilishi pekee wa soka la Wanawake mkoa wa Shinyanga, Shinyanga Super Queens yanazidi kupamba moto kwa ajili ya Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara (WFDL) inayotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Shinyanga Super Queens baada ya kuangukia pua katika mchezo uliopita wa kirafiki dhidi ya ES Unyanyembe ya Tabora kwa kutandikwa mabao 5-3 kwenye dimba la CCM Kambarage, mjini Shinyanga, leo Jumapili walijitupa tena uwanjani hapo kujaribu makali yake na silaha mpya walizozipata.

Ambapo waliwakaribisha Vijana wenye umri chini ya miaka 17 wa Kituo cha Soka cha Moroto cha mjini Shinyanga, na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, huku mabao yote ya Shinyanga Super Queens yakipachikwa nyavuni na mshambuliaji wao, Irine Chitanda (Messi).

Mchezo huo ambao ulikuwa maalum kwa ajili ya tukio la uzinduzi wa jezi zao mpya walizokabidhiwa kutoka Kampuni ya Jambo Food Product, ulihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko na baadhi ya viongozi wa serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiwemo Mkurugenzi wa Thubutu Africa Initiative, Jonathan Manyama.

Baada ya mchezo huo, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko aliwapongeza viongozi wa timu hiyo kwa kukuza na kuendeleza vipaji vya watoto wa kike na kuwataka waendelee kukazania mazoezi ili kuwa imara zaidi.

Pia, DC Mboneko aliahidi kuwakabidhi Mbuzi (mnyama) wawili na Sh 100,000 kwa ajili ya safari yao ya maandalizi, huku akiahidi Mbuzi mmoja kwa timu ya Moroto FC.

Mkurugenzi wa Shinyanga Super Queens, Flora Gaguti amewashukuru wadau wote amabo wameendelea kuisaidia na kuinga mkono timu yake katika maandalizi hayo ya michuano ya ligi daraja la kwanza, huku akiendelea kuwakaribisha wananchi kuunga mkono safari yao ya kuelekea kwenye michuano hiyo.

Naye Ofisa Michezo na Utamaduni wa Halmashauri ya Shinyanga, Mankiligo alitoa Sh 20,000 kwa timu hizo, huku Jonathan Manyama akitoa Kisanduku cha dawa chenye thamani ya Sh 50,000 na Mbuzi mmoja kwa timu ya Shinyanga Super Queens na Sh 10,000 kwa Moroto FC.

Kwa upande wa kampuni ya Jambo Food Products ambao ndiyo wadhamini wa jezi za Shinyanga Super Queens, kupitia kwa Afisa Masoko wake, Ophebia Juvenary wameahidi kujitolea vinywaji na maji kwa timu hiyo kwa kila mchezo watakaocheza.

Mratibu wa Mratibu wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF Iliyoboreshwa) Manispaa ya Shinyanga, Jackson Njau ambao waliwezesha mchezo huo, amewahimiza wananchi kujiandikisha na huduma hiyo ili kupunguza gharama za matibabu kwenye kaya zao

DC Mboneko akipiga mpira kuelekea golini kuashiria ufunguzi wa mchezo huo
 
 
DC Mboneko akikagua vikosi na kusalimiana na wachezaji kabla ya kuanza mchezo

DC Mboneko akionyesha jezi maalum zitakazotumiwa na timu ya Shinyanga Super Queens kwenye mashindano mbalimbali ambazo zimezinduliwa leo uwanjani hapo

 Beki wa timu ya Shinyanga Super Queens akijaribu kuondoa mpira kwenye eneo lake wakati wa mchezo huo wa kirafiki
 
Nahodha wa Shinyanga Super Queens, Tatu Abbas akiwatoka wachezaji wa Moroto FC katika mchezo wa kirafiki uliozikutanisha timu hizo 
 
Mchezaji wa Moroto FC akiwatoka wachezaji wa Shinyanga Super Queens
 
DC Mboneko pamoja na viongozi wengine wakifuatilia mchezo huo
Kikosi cha Shinyanga Super Queens

Kikosi cha akiba cha Shinyanga Super Queens
Benchi la ufundi la timu ya Moroto FC likizungumza na wachezaji wakati wa mapumziko kujaribu kutoa maelekezo.

Kocha Msaidizi wa Shinyanga Super Queens, Suleman Shaban Hamad akizungumza na wachezaji wakati wa mapumziko



Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akiserebuka pamoja na wachezaji wa timu ya Shinyanga Super Queens baada ya ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Moroto FC leo kwenye uwanja wa Kambarage, Shinyanga

DC Mboneko akizungumza na wachezaji baada ya mchezo huo





DC Mboneko akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa Shinyanga Super Queens

DC Mboneko akiwa katika picha ya pamoja na waamuzi waliochezesha mchezo huo

Mratibu wa CHF iliyoboreshwa Manispaa ya Shinyanga, Jackson Njau akizungumza baada ya mchezo huo

Mkurugenzi wa Shinyanga Super Queens, Flora Gaguti akizungumza

Furaha ikiwa imetawala kwa timu ya Shinyanga Super Queens
Afisa Masoko wa Jambo Food Products, Ophebia Juvenary akizungumza kwenye mchezo huo

Jonathan Manyama ambaye ni mdau wa maendeleo mkoani Shinyanga akitoa ahadi ya Mbuzi mmoja kwa timu ya Shinyanga Super Queens

Afisa Michezo na Utamaduni Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Said Mankirigo akizungumza na wadau pamoja na wachezaji walioshiriki katika mchezo huo

Baadhi ya Mashabiki waliojitokeza kuushuhudia mchezo huo

Mashabiki wakiendelea kupata burudani

DC Mboneko na viongozi wengine wakiendelea kufuatilia mchezo huo katika uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga


Nahodha wa Moroto FC, Ferouz Siraji

Nahodha wa Shinyanga Super Queens, Tatu Abbas
DC Mboneko akiondoka uwanjani baada ya kuufungua mchezo

DC Mboneko katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali waliohudhuria mchezo huo



 DC Mboneko alipata pia fursa ya kupiga picha na waandishi wa habari waliofika kuushuhudia mchezo huo.