Header Ads Widget

POLISI MOSHI YASEMA IMEWAKATA WALIOMPIGA MAWE LISSU

JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro limewakamata watuhumiwa 12 wanaodaiwa kufanya vurugu za kushambulia kwa mawe, mkutano wa mgombea Urais kupitia Chadema, Tundu Lissu.
Katika taarifa yake iliyotolewa hii leo Agosti 23, 2020, Kamanda wa Polisi mkoani  Kilimanjaro, ACP Emmanuel Lukula alisema kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 14 mwaka huu, ambapo katika mahojiano yao na vijana hao wamedai kuwa kulikuwa na mtu nyuma yao ambaye amekimbia.
"Tumetumia sana intelejensia ya Polisi ili kuwabaini hao watu waliofanya kitendo hicho cha aibu kubwa tumefanikiwa kuwapata 12, wengine tumewakamatia Arusha wanasema baada ya hilo tukio waliona kama wangerudi majumbani mwao wangekamatwa, tumewafuatilia kwa muda mrefu lakini tumeona tuwafuate walipo, mbaya zaidi wanatueleza kuwa kuna mtu aliyekuwepo nyuma yao na amekimbia" amesema Kamanda Lukula.
Aidha Kamanda Lukula ametahadharisha vijana watakaotumika kisiasa kuvurugu amani katika mikutano mbalimbali ya vyama vya siasa mkoani kilimanjaro watajikuta kwenye mikono ya sheria.