Header Ads Widget

WANA CCM 129 WACHUKUA FOMU WILAYA YA KAHAMA KUCHUANA NA KWANDIKWA, MAIGE NA KISHIMBA



 Mmoja wa wanachama wa CCM waliojitokeza leo kuchukua fomu ya kuwania ubunge katika jimbo la Kahama Mjini, James Lembeli

Salvatory Ntandu- Kahama (UMG)
Jumla ya Watia nia 129 kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamejitokeza kuomba ridhaa ya kuchaguliwa kugombea nafasi ya Ubunge katika majimbo ya Msalala, Ushetu na Kahama Mjini tangu kuanza kwa zoezi la utoaji fomu lililoanza Julai 14, 2020 likitarajiwa kuhitimishwa Julai 17 Saa 10 jioni.

Akizungumza leo Julai 16, 2020 ofisini kwake na waandishi wa habari mjini Kahama mara baada ya kuhitimisha siku ya pili ya zoezi la utoaji wa fomu, Katibu wa CCM wilaya ya Kahama, Emmanuel Mbamanga amesema zoezi hilo linazidi kuwavutia makada wengi zaidi ambao wamejitokeza kuomba nafasi za ubunge katika majimbo hayo.

Amesema Jimbo la Kahama Mjini ndio linaongoza kwa kuwa na watia nia wengi ambapo mpaka leo Jioni kulikuwa na wagombea 69 waliokweisha chukua fomu 40 tayari wamekwisha zirejesha huku 29 wakiwa bado hawajazirushisha na idadai ya wanawake waliojitokeza ikiwa ni nane.

Mbamange amefafanua kuwa Katika Jimbo la Msalala jumla ya watia nia 43 wamekwisha chukua fomu za kuomba nafasi ya ubunge ambapo wanaume ni 42 na mwanamke mmoja huku waliokwisha rudisha fomu ni 31 na ambao bado ni 13.

Wakati katika jimbo la Ushetu, jumla ya watia nia 17, wakiwemo wanaume 15 na wanawake wawili wamejitokeza, huku waliorudisha fomu wakiwa 14, huku asilimia 80 ya waliochukua fomu katika majimbo yote matatu wengi wao wakiwa ni vijana.

Ameongeza kuwa mabadiliko ndani ya CCM mpya chini ya Mwenyekiti  wa CCM taifa, Dk John Magufuli  yamewavutia na kuwahamasisha vijana wengi kukipenda chama kutokana na kazi zilizotekelezwa kwa awamu ya tano .

Mwenyekiti wa KACU, Emmanuel Charahani nae amechukua fomu ya kugombea ubunge wa Jimbo la Ushetu.