Header Ads Widget

MEMBE ATAMBULISHWA RASMI KWA WANACHAMA, ADAI NDOTO YAKE SASA ITATIMIA

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika serikali ya awamu ya nne, Bernard Membe leo Julai 16, 2020 ametambulishwa rasmi mbele ya wanachama wa chama cha ACT -Wazalendo kama mwanachama mpya.
Akizungumza mara baada ya kukaribishwa na kutambulishwa kwa wanachama wa chama hicho, Bernard Membe amesema kabla hajafikiria kujiunga na chama hicho alisoma katiba yao na kuielewa na kwa maono yake anasema ACT ndicho chama pekee cha upinzani kinachokua kwa kasi hapa nchini.
"Nataka kupigania mabadiliko ya kweli ya hii nchi kupitia ACT azma yangu itatimia," amesema Membe.
CHANZO: CLOUDS TV